Ads

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AMUAPISHA IDD HASSAN KAMANTA KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Idd Hassan Kamanta kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Juni 2020
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Idd Hassan Kamanta akila kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare akimuapisha Bakari Msulwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Ikulu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya pamoja na Wakurugenzi wakila kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mkuu wa Mkoa wa Arusha Idd Hassan Kamanta akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Laban Kihongosi Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Juni 2020.Picha na Ikulu

No comments