Ads

Korea Kaskazini yalipua ofisi ya pamoja na Korea Kusini....Jeshi Lawekwa Katika Hali Ya Tahadhari


Korea Kaskazini imesema inaliweka jeshi lake katika hali ya tahadhari ya kivita, ikiwa ni muda mfupi baada ya kulipua ofisi ya pamoja kati yake na Korea Kusini, ikiituhumu Korea Kusini kuruhusu wanaharakati kurusha maputo yenye ujumbe wa uchochezi kuelekea kaskazini.

Makao ya Ofisi hiyo iliyofunguliwa Septemba 2018 kama sehemu ya makubaliano kati ya kiongozi wa kaskazini Kim Jong Un na Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini yalikuwa katika mji wa Kaesong, ulio kaskazini.

Mkuu wa jeshi la Korea Kaskazini amesema wanaandaa mpango mkakati wa kuingia maeneo ambayo yaligeuzwa kuwa yasiyo na shughuli za kijeshi mwaka 2018, akitishia kuyageuza magofu.

Jengo hilo la ghorofa nne lilikuwa linatumiwa na kampuni kadhaa za Korea Kusini, ambazo zimeajiri wafanyakazi kutoka Korea kaskazini, na ambao mishahara yao hulipwa kwa serikali ya Korea Kaskazini.

No comments