WANANCHI WAMESHAURIWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KUPAMBANA NA COVID_ 19.
Mwambawahabari
Shirika la Elimu ya Amani (EA) imewashauri wananchi kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na kuzuia Ugonjwa wa Covid_19 kwa kufuata kanuni za afya ikiwa na lengo la kutokomeza Ugonjwa huo.
Rai hiyo imetolewa leo Jijin Dar es salaam na Rais wa Shirika la Elimu ya Amani Wilson Munguza katika uzinduzi wa zoezi la uhamasishaji kujikinga na Ugonjwa wa Korona ikiwemo uvaaji wa barakoa.
Munguza amesema watu wanatakiwa kufuata Sheria na kanuni za afya ikiwa ni Juhudi za kupambana dhidi ya ugonjwa wa Korona.
"Leo tumezindua zoezi la ukaguzi uvaaji wa barakoa ni mkakati madhubuti utakaofanyika nchi nzima, nawasihi Watanzania kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa taarifa kutoka Serikalini na wataalamu wa afya." Amesema.
Aidha Anthony Mkama ni mwenyekiti wa Shirika la Elimu ya Amani Afrika Mashariki amesema kuwa zoezi la ukaguzi wa uvaaji barakoa litakuwa endelevu hadi Ugonjwa huo utakapo isha nchini.
Hata hivyo ametoa Rai kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadahari wao wenyewe pasipo kushurutishwa na mtu yeyote katika kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Korona,ikiwa ni jukumu la kila mmoja kutokomeza maambukizi mapya ya ugonjwa huo.
"Naishauri serikali suala hili liwe endelevu hadi Ugonjwa wa Korona utakapopotea, watu wajikinge na ugonjwa huu kwa kufuata maelekezo kutoka kwa wataalamu wa afya, ni wajibu wetu kuungana kwa pamoja kufanikisha ugonjwa huu usiendelee kutuletea madhara." Amesema.
Kwa upande wake Judith Nzala Msemaji Mkuu wa Muungano amesema kuwa katika zoezi la uhamasishaji wamekumbana na Changamoto ya baadhi wa watu kuwa na uelewa mdogo jinsi ya kujikinga na Korona na wengine kukataa kuvaa barakoa kwa mujibu wa imani zao.
"Tumekumbana na Changamoto nyingi ikiwemo watu kutokana na imani zao kukataa kuvaa barakoa wakidai kuwa hawataweza kuambukizwa, lakini Sisi wanashirika tunashauri watu wote popote walipo wazingatie maagizo yatolewayo na serikali na wataalamu wa afya namna ya kujikinga na Ugonjwa wa Korona." Amesema
Nae Samila Ngingo Mratibu wa Sanaa na Utamaduni wa Shirika hilo amesema kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa na mapokeo hafifu ya taarifa juu ya ugonjwa wa Korona kwani Kuna baadhi ya watu hawavai barakoa na watoto wengi wanadhurura barabarani na wanatumika kufanya biashara barabarani, amewashauri wazazi waangalie watoto kwa umakini wasiwaachie watoto kudhurura barabarani.
"Nimeona kuna watoto wako barabani wanadhurura na wengine wanafanya biashara barabarani kwenye magari, kutokana na hili janga la Korona nawasihi wazazi wenzangu wasiwaruhusu watoto kudhurura ovyo barabarani na kufanya biashara kwenye mikusanyiko ya watu, tuzingatie maelekezo ya Serikali na wataalamu wa afya wanachotuelekeza." Amesema.
Shirika la Elimu ya Amani kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzia na usalama leo wameanza zoezi la uhamasishaji kujikinga na Ugonjwa wa Korona kwa kuingia kwenye magari ya usafiri wa umma kuhamasisha abiria na wafanyabiashara kuvaa barakoa na kufuata kanuni za afya ikiwa na lengo la kuzuia maambuzi mapya ya ugonjwa huo ambapo ni Juhudi za kuunga mkono serikali kupambana dhidi ya ugonjwa wa Covid_19.
Post a Comment