Ads

UGONJWA WA CORONA ISIWE KIKWAZO CHA KUTUKWAMISHA KIUCHUMI : MKUVASA



Kutokana na Dunia kuingia taharuki ya ugonjwa wa Korona na kusababisha mtikisiko wa  kiuchumi na kusababisha watu kuwa na hofu ya kudorora kiuchumi Shirika la Elimu ya Utunzaji wa Amani nchini imewataka Watanzania kuondoa hofu ya kudhorota kiuchumi bali wakijikite kufanya kazi kwa bidii na kutumia ubunifu zaidi kukuza na kuendeleza maendeleo ya kiuchumi.


Wito huo umetolewa leo Jijini Dar salaam na Afisa Mahusiano Kimataifa Shirika la Elimu ya Utunzaji wa  Amani Charles Mkuvasa wakati akifanya mahojiano na Mwandishi wa habari amesema, katika kipindi hiki Cha Janga hatari la Ugonjwa wa Korona kumekuwa na Changamoto nyingi ikiwemo mdororo wa  kiuchumi.

Kutokana na kuwepo na mtikisiko wa kiuchumi na kusababisha watu kuwa hofu ya kudorora kiuchumi Mkuvasa amewataka wananchi kugeuza Changamoto kuwa fursa ili kupambana hali tete ya kiuchumi.

"Changamoto hii tuliyonayo ya Janga Hili la Ugonjwa wa Korona isiwe kikwazo  cha kutukwamisha  kiuchumi bali hii tunaweza  kubadilisha Changamoto hii kuwa fursa kwa kufanya ubunifu kuhakikisha tunajikwamua kiuchumi." Amesema.

Kwa upande wake Afisa Mahusiano Kitaifa Renben Kimbe amesisitiza watu wasiwe na hofu na Ugonjwa wa Korona bali wachukue tahadahari dhidi ya COVID_19 na kufanya kazi kwa bidii katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda, biashara, kilimo nakadhalika.

Amesema watu waendelee kujikita zaidi kufanya shughuli za uzalishaji kiuchumi  ili kusaidia kurudisha hali ya kiuchumi kurejea kama awali ambapo ni katika muendelezo wa Juhudi za Serikali Tanzania kufikia Uchumi wa Kati hadi mwaka 2025.


"Watanzania wanatakiwa waendelee kuchukua tahadahari dhidi ya ugonjwa wa Korona lakini pia waendelee kufanya kazi, Kuna baadhi ya Mataifa wamesimama kufanya kazi lakini sisi tuendelee kuchapa kazi katika maendeleo ya kiuchumi ikiwa ni maono  ya Serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli Tanzania kufikia Uchumi wa Kati ifikapo mwaka 2025.

Aidha Shirika la Elimu ya Utunzaji wa Amani imetoa  pongezi kwa Serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kuhakikisha kwamba Watanzania kubaki kuenzi Amani tuliyonayo.

Pia pongezi imetolewa  kwa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kwa jitihada kubwa ambayo imechukua kwa mapana yake kwa kutumia Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa jitihada nzuri ambayo wameifanya katika kuhakikisha Dunia kubaki kuwa na Amani kurudi katika wakati wa mwazo.

No comments