Ads

TAASISI YA MO DEWJI KWA KUSHIRIKIANA NA SIMBA SPORT CLAUB YATOA MSAADA VIFAA KUJIKINGA NA CORONA.

Meneja Mradi wa Taasisi ya Mo Dewji Bi Rachel Chengula akizungumza jambo na wafanyabiashara wa soko la Mabibo jijini Dar es Salaam.
Na Iddi Iddi, Dar es Salaam.
Taasisi ya Mo Dewji kwa kushirikiana na kabla ya Simba imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya kujikinga na ugonjwa wa virusi vya corona katika katika masoko tofauti katika jijini la Dar es Salaam.

Vifaa hivyo vya kujikinga na virusi vya corona ni pamoja na barakoa, sabuni pamoja na vitakasa mikono.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Mei 18, 2020 wakati akikabidhi vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa corona katika soko la Mabibo, Meneja Mradi wa Taasisi ya Mo Dewji Bi Rachel Chengula, amesema lengo ni kuwasaidia wananchi kujikinga na ugonjwa wa corona.
Bi Chengula amesema kuwa katika soko la mabibo wametoa vifaa tafauti vya kuzuia maambuziki ya virusi vya corona ikiwemo barakao 1,000.
“Tunaendelea kugawa msaada katika masoko mengine ili tuwezea kutoa barakoa 25,000 pamoja na vifaa vingine vya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona” amesema Bi Chengula.

Project Meneja wa klabu ya Simba amesema kuwa lengo ni kuwafikia watu wenye kipato cha chini ambao hawajiwezi kiuchumi hasa wafanyabiashara wadogo.

 Amesema kuwa wamekuwa wakizunguka katika maeneo tofauti ili kuwafikia moja kwa moja walengwa na kuwapatia msaada huu ikiwemo madereva wa pikipiki.
Kwa upande wake Meneja wa Soko la Mabibo Bw. Moses Waromi, ameishukuru Taasisi ya Mo Dewji na klabu ya simba kwa kuwakumbuka kwa msaada wa vifaa vya kujikinga na corona.

Ameeleza kuwa msaada huo unaonesha ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana maambukizi ya virusi vya corona.
 


No comments