Ads

MUNGUZA AMETOA WITO KWA WANANCHI KUTOKUKUSANYIKA KATIKA KUSHEHEREKEA SIKUKUU YA EID EL FITRY ILI KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA CORONA.



Mwambawahabari


.................................................................


Shirika la Elimu ya Amani (EA) linamuunga mkono Mkuu wa Jeshi la Polisi  Nchini, (IGP) Simon Sirro kwa kupiga marufuku kufanya sherehe na kwenda kwenye kumbi za starehe na mikusanyiko mbalimbali katika kipindi hiki Cha Sikukuu. 

Hayo ameyasema leo Ofisi ndogo ya Makao Makuu Jijin Dar es salaam Rais wa Shirika la Elimu ya Amani Wilson G. Munguza amesema, katika kipindi hiki cha sikukuu ni jambo jema watu  kutokukusanyika na kufanya masherehe ikiwa ni njia ya kujiepusha na maambukizi ya Virus vya Korona.

Munguza amesema katika kipindi hiki Cha Sikukuu watu wanatakiwa kujiepusha kwenda kwenye kumbi za starehe, masherehe, na mikusanyiko mbalimbali ili kuzuia athari ya maambukizi mapya ya Korona .

"Namuunga mkono Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro kwa kupiga marufuku watu kutojihusisha na mikusanyiko na kwenda wenye kumbi za starehe ikiwa na lengo la kuzuia na kupambana dhidi ya ugonjwa wa Korona hata hivyo itasaidia kupunguza vitendo vya uvunjifu wa amani ikiwa watu wanasheherekea sikukuu wakiwa nyumbani." Amesema. 

Mshauri wa Ofisi ya Rais Shirika la Elimu ya Amani Salehe Ally Tengeneza amewashauri wananchi kuchukua tahadhari kutokana na vitendo vya wizi kipindi hiki Cha Sikukuu kulinda mali zao, pia amewataka watu kutojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani.

"Kipindi hiki Cha Sikukuu kuna matukio mengi ya uvunjifu wa amani ikiwemo wizi na utapeli watu wanatakiwa kuwa makini kulinda mali zao na nawasihi watu kutojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani" Amesema

No comments