MCHUNGAJI MKAMA AMEWATAKA WATANZANIA KUENDELEA KUFANYA MAOMBI.
Mchungaji wa Kanisa Evangelistic Assemblies of God Tanzania [EAGT] Anthony James Mkama amewataka watanzania kuendelea kufanya maombi na kufanya ibada huku wakichukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Korona kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizowekwa Serikali na wataalamu wa afya ili kupambana na ugonjwa huo.
Amezungumza hayo leo Jijini Dar es salaam amesema kadri tunavyoendelea kufanya maombi ndipo Janga hatari la Korona litaendelea kupungua, hivyo watu wanapaswa kufanya maombi kwa bidii na kuzingatia taratibu zilizowekwa na wataalamu wa afya kujikinga na Ugonjwa wa Covid_19.
"Kadri tunavyozidi kuendelea kuomba ndivyo makali ya Korona yanaendelea kupungua pia tuzingatie Sheria na taratibu tunazopewa na viongozi wetu" Amesema.
Mchungaji Anthony amesisitiza waumini wa dini zote kuungama dhambi kuacha kufanya maovu bali washikamane kufanya kazi kwa bidii na kuishi wa amani.
Aidha amesema watu waache kutoa taarifa za upotoshaji na kuharibu amani bali watu wanatakiwa kusema maneno yenye tija ya malengo ya kuleta maendeleo nchini.
"Watu itakiwa tujenge msingi mzuri katika jamii yetu tuzungumze maneno yenye umuhimu yenye kujenga na kutuimarisha kiroho, kiuchumi, kisiasa nakadhalika".
Pia ameishukuru Serikali kwa kuruhusu shughuli za ibada ziendelee kufanyika kama kawaida hivyo kuwasihi waumini wa dini zote ziendelee kufuata maelekezo yalitolewa na Serikali kwa kuendelea kuchukua hatua za kujilinda na Ugonjwa wa Korona.
"Nichukue fursa hii kumshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa kutaka nyumba za ibada zisifungwe ili watu waendelee kumuomba MUNGU atuepushe na Janga Hili la Korona". Amesema.
AMENI Baba
ReplyDelete