KAMPUNI YA FMJ HARDWARE YATANGAZA MNADA MKUBWA KUWASAIDIA WANANCHI KUMILIKI NYUMBA.
Meneja Mauzo Kampuni
ya Uuzaji wa Vifaa vya Ujenzi FMJ Hardware Limited Bw. Fredrick Ally Sanga akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Mauzo Kampuni ya Uuzaji wa Vifaa vya Ujenzi FMJ Hardware Limited Bw. Fredrick Ally Sanga akionyesha baadhi ya vifaa vya ujenzi ambavyo vinatarajiwa kupigwa mnada Mei 30 mwaka huu.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Kampuni ya Uuzaji wa Vifaa vya Ujenzi FMJ Hardware Limited iliyopo Buguruni
Kisiwani jijini Dar es Salaam inatarajia kufanya mnada wa moja kwa moja siku ya Mei 30
mwaka huu kupitia yombo vya habari (Online Media).
Mnada huo unatarajia kufanyika katika ofisi ya Kampuni hiyo iliyopo Buguruni
Kisiwani mkabala na barabara ya mandela jijini Dar es Salaam ambapo vifaa
mbalimbali vya ujenzi ikiwemo rangi, nondo, bati vitapigwa mnada kwa gharama nafuu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Meneja
Mauzo Kampuni ya Uuzaji wa Vifaa vya Ujenzi FMJ Hardware Limited Bw. Fredrick
Ally Sanga, amesema kuwa lengo la mnada huo ni kumuwezesha mwananchi aweze
kufikia ndoto zake za kumiliki nyumba kwa gharama nafuu.
Amesema kuwa katika mnada huo kutakuwa na vifaa vya ujenzi bora venye
gharama nafuu ambapo itakuwa ni sehemu ya kuunga mkono kauli ya Rais Dkt. John
Pombe Magufuli katika kuhakikisha watu wanafanya kazi huku wakiendelea
kujingika na ugonjwa wa homa kali ya mapafu corona.
“Mnada huu utasaidia kuepuka mikusanyiko katika kufanya biashara,
ndiyo maana kampuni hii ya FMJ Hardware Limited ikaona ikufikishie na
ikurahisishie wewe mwananchi kuagiza bidhaa zako utakazo hijitaji na kununua
kwa njia rahisi kupitia mnada wa online media ukiwa umetulia nyumbani kwako
ukifatilia pamoja na kufata kanuni za kujikinga na corona kwa kuepuka msongamano”
amesema Bw. Sanga.
Ameeleza kuwa mnada huo utaanza saa 6 mchana mpaka saa 9 alasiri ambapo utakuwa mubashara (live) kupitia online media ikiwemo Ayo Tv, Global Tv, Michuzi Tv, Tanzanite Tv, Dar Mpya Tv, Icon Tv, Javi Tv pamoja na vyombo vingine vya habari.
Hata hivyo Bw. Sanga amewakaribisha wananchi wote kufatilia mnada huo na kununua vifaa vya ujenzi kwa kupiga simu kupitia namba 0653 312 438, 0716 902 995 pamoja na kuwasiliana nao kupitia mtandao wa kijamii facebook Fmj hardware.
Post a Comment