MAJALIWA MGENI RASMI KONGAMANO LA KIBIASHARA
Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Kibiashara kati
ya Wafanyabiashara watanzania na Wafanyabiashara wenye makampuni kutoka nchini
Sweden litakalofanyika jijini Dar es Salaam Machi 12 hadi 13 mwaka huu.
Akizungumza
na wanahabari jana jijini humo Rais wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda
na Kilimo Tanzania (TCCIA), Paul Koyi alisema kongamano hilo la siku mbili
litakutanisha wafanyabiashara wa nchini na kutoka Sweden lengo likiwa kuangalia
fursa za uwekekezaji katika sekta zote ikiwemo viwanda, biashara na kilimo.
“Tunatarajia
Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Mkuu kongamano hili litaleta msukumo wa kibiashara
litawasaidia wafanyabiashara kuchangamkia fursa za uwekezaji kwa kushirikiana
na wenye makampuni Wasweden,” alisema.
Alibainisha
kuwa mwaka jana kongamano lilifanyika katika Mji wa Stockholm na kwamba mwakani
litafanyika Rwanda huku akisisitiza limedhamiria kutekeleza sera ya uchumi wa
viwanda ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dkt. John Magufuli.
Aliwaomba
wafanyabiashara wote waliojiandikisha kuhudhuria kongamano kwani litawafungulia
fursa nyingi za kibiashara watapokutana na wenye makampuni kutoka Sweden.
Kwa upande
wake Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt. Wilbrod Slaa alisema Wafanyabiashara
Wasweden wenye makampuni hawawezi kuwekeza peke yao bali wanapenda kuwekeza kwa
mtindo wa ushirikiano.
Alizitaja
miongoni wa kampuni kutoka nchini humo zitakazoshiriki ni Kampuni ya Volvo
inayojishughulisha na utengenezaji wa magari madogo na makubwa pamoja na
Kampuni ya Apple Energy.
Mwenyekiti
wa Chemba hiyo kutoka Sweden upande wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
(SWEACC), Jan Furuvald alisema kongamano litafungua fursa za kibiashara kupitia
uwekezaji wa sekta mbalimbali utakaojumuisha watanzania na Wasweden.
Post a Comment