Ads

Mufti Mkuu Wa Zanzibar Aongoza Dua Maalum Ya Kuiomba Nchi Na Maradhi Ya Corona

SHEIKH Dkt. Muhidin Ahmady (Mwalim Siasa) akisoma dua wakati wa Dua Maalum ya kuiombea Nchi kutokana na Maradhi ya Corona (CODIV -19) kulia Sheikh Shaban Ali Batashi, Mshauri wa Waziri wa Sheria na Katiba Sheikh Fadhil Soraga na Sheikh. Said Suleiman wakiitikia dua hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa ZBC Karume house jana usiku.(Picha na Othman Maulid).

MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akisoma dua maalum ya kuiomba Nchi kutokana na Maradhi ya Corona, iliyofanyika kupitia vyombo vya habari vya ZBC TV na Redio na kurushwa moja kwa moja kwa wananchi, (kushoto kwa Mufti) Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar.Sheikh. Hassan Othma Ngwali na (kulia kwa Mufti) Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar.Sheikh Mahmoud Mussa Wadi, wakiitikia dua hiyo, ilioyofanyika katika ukumbi wa Kituo cha ZBC mnazi mmoja Jijini Zanzibar jana usiku.(Picha na Othman Maulid)
SHEIKH Abdulraham Sheikh Al-Habshi akisoma dua maalum ya kuiombea Nchi kutokana na Maradhi ya Corona iliyofanyika kupitia chombo cha habari cha ZBC TV na Redio na kurushwa moja kwa moja jana usiku, (kushoto kwake)Sheikh. Samir Zukfika Ramdhan na Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume.(Picha na Othman Maulid)
NAIBU Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Hassan Othman Ngwali akisoma dua wakati wa hafla ya kuiombea Nchi Dua ya kutokana na Maradhi ya Corona yalioikumba dunia, dua hiyo imefanyika kwa njia ya Vyombo vya Habari vya ZBC Tv na Redio, katika kituo hicho Karume House Mnazi mmoja Jijini Zanzibar, (kulia) Mufti Mkuu wa Zanzibar. Sheikh Saleh Omar Kabi na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Skheih Mahmoud Mussa Wadi.(Picha na Othman Maulid)


MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi,akiongoza dua Maalum ya kuiombea Nchi kutokana na Maradhi ya Corano,iliofanyika kwa njia ya vyombo vya habari katika ukumbi wa ZBC Karume House Zanzibar jana usiku na kuoneshwa moja kwa moja, (kushoto kwa Mufti) Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Hassan Othman Ngwali na ( kulia kwa Mufti) Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar.Sheikh. Mahmoud Mussa Wadi, wakiwa na masheikh wengine wakiitikia dua hiyo iliofanyika jana usiku.(Na.Othman Maulid)

No comments