HAWA HAPA VIONGOZI WAPYA WA ACT- WAZALENDO
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Wajumbe wa
Mkutano Mkuu wa Chama ACT Wazalendo wamemchagua Maalim Seif kuwa Mwenyekiti wa
Chama hicho baada ya kupata kura 337 sawa na asilimia 93.3 katika uchaguzi unaoendelea
wa kuchagua viongozi ngazi ya taifa.
Wajumbe wa
mkutano huo wameonekana kuwa na furaha baada ya matokeo kutangazwa, Maalim
Seif kabla ya kuchaguliwa uenyekiti alikuwa Mshauri Mkuu wa Chama hicho.
Akitangaza
matokeo hayo leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Kamati maalumu ya uchaguzi
ACT- Wazalendo Omary Shabaani, amesema kuwa jumla ya wajumbe 375 walioshiriki
katika uchaguzi ni 375, kura halali zilikuwa 367 huku kura 4 zikiharibika.
Viongozi
wengine waliochaguliwa ni pamoja na Bw. Zitto Kabwe amechaguliwa kuwa kiongozi
Mkuu wa Chama, Bw. Juma Haji ni makamu mwenyekiti upande wa Zanzibar, Bi
Dorotha Semu ni Makamu mwenyekiti Tanzania bara.
Uchaduzi huo
unaendelea kwa kuchagua viongozi mbalimbali ikiwemo wajumbe wa Halmashauri Kuu
ya Taifa pamoja na kamati kuu ya Chama, wajumbe watakaopatikana kesho machi 16
mwaka huu watapiga kura kumchagua katibu mkuu wa chama pamoja na manaibu wake.

Post a Comment