Ads

DC DKT MJEMA AHAMASISHA WANANCHI KUHUSU KUJIKINGA NA UGONJWA WA CORONA .


Na John Luhende
Mwamba wa habari
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Dkt Sophia Mjema leo amewataka wananchi wa Wilaya ya Ilala na wale wanaoingia  wilayani humo  kuzingatia kanununi za afya na maelekezo ya wataalam wa afya  ili kuweza kujikinga na ugonjwa wa CORONA.

Dkt Mjema  ameyasema hayo  leo wakati wa  ziara ya kuhamasisha  na kutoa elimu kwa  wananchi kuhusu kujikinga na ugomjwa wa Colona  unaoenezwa na Virurusi vya COVID 19 .
Aidha DC Dkt Mjema ametembelea maeneo ya Kariakoo sokoni,Bandari ya boti za kwenda Zanzibari,Soko la Ferry  na maeneo mengine yenye mikusanyiko  na kuhamasisha wananchi kunawa mikono kwa dawa maalumu ambapo pia aliwanawisha  .

"Tunawaagiza wasimamizi wa vyombo vyote vya kubeba abiria  kwamba zoezi hili niendelevu wahakikishe wanasafisha kwa dawa vyombo vyao"Alisema

Kwa upande wake Afisa afya wa Manispaa ya Ilala Reginald Mlai , amesema kunawa mikono pekee haitoshi ila wananchi pia wanatakiwa kufunika midomo wakati wa kukohoa.

Nao baadhi ya wananchi waliopewa elimu hiyo wamemshukuru Mjema  kwa kwa kuwajali wananchi huku wakiomba Serikali kuongeza juhudi katika ktoa elimu kwani wananchi wengi hawanauelewa kuhusu ugonjwa huo.

"Sisi wafanya biashara ndogondogo tunaomba Rais atufanyie mpango wa kununua maski maaana  zimekuwa beighali sana"alisema  mmoja wa wafanyabiashara ndondogo Kariakoo.

No comments