CUF YAIPONGEZA SERIKALI KATIKA JUHUDI ZA KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA

Katika kupambana na kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa CORONA unaosababishwa na virus vya COVID 19 , Chama cha wananchi CUF kimeitaka serikali kuongeza udhibiti katika njia zote za usafiri ili kuzuia maambukizi kuenea.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Haruna Lipumba wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuhusu tishio la ugonjwa huo.
Pia amesema kwakuzingatia tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona na ushauri wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na agizo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chama kimeamua kusitisha ziara zote za mwenyekiti wa chama Taifa kwa mwezi mmoja.
“Baraza kuu la Uongozi la Taifa liliishauri Serikali kuongeza uwezo wa kupima maradhi ya COVID 19 hasa katika viwanja vya ndege vya kimataifa ,hospitali na vituo vya afya kuweka taratibu za karantini,wadi za kulaza na katibu wagonjwa ikiwa ugonjwa utaibuka”amesema Prof Lipumba.
Prof Lipumba amesema Serikali kwa kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa hasa WHO iandae mkakati madhubuti wa kukabiliana na mlipuko wa COVID 19.
Vilevile ameitaka serikali kupitia kadhia ya virusi vya Coronakujifunza ili kujenga mfumo imara wa huduma za afya za msingi na amesisitiza kinga ya maradhi ni kuishi katika mazingira safi.
Aidha chamahicho kimetoapongezi kwa juhudi ambazo Serikali imechukua katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona ikiwa ni pamoja na kutangaza mara kwa mara njia za kudhibiti na hatua za dharura za kuchukua pindi dalili zinapodhihirika.
Sanjari na hayo amesema Chama Cha wananchi CUF kinato wito kwa Vingozi wa Dini kuongeza Dua na maombi ili Mungu awape nafuu kwakuzingatia hali ya maisha ya Watanzania walio wengi ni rahisi sana ugonjwa huu kuenea kwa kasi kupitia vyombo vya usafiri.
“Tunatoa wito kwa wananchi wote kuzingatia maelekezo ya kitaalam ya kujikinga na maambukizi ya maradhi haya”amesema Prof Lipumba.
Post a Comment