Ads

Brigedia Jenerali John Mbungo aula TAKUKURU

Rais Magufuli amteua Brig. Jenerali John Mbungo kuwa Mkurugenzi wa TAKUKURU
Rais wa Jamhuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amthibitisha Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) Brig. Jenerali John Mbungo kuwa Mkurugenzi wa taasisi hiyo baada ya kuokoa Sh bilioni 8.8 za wakulima.

Rais amefanya uteuzi huo baada ya kupokea ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2018/2019 inayowasilishwa na Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Seriakali (CAG) Charles Kichere na ripoti ya taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya mwaka 2018/2019 itakayowasilishwa na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Taasisi hiyo Brigedia Jenerali John Mbungo .
Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo Machi 26, 2020.

No comments