Ads

YANGA WALAZIMISHWA SARE NYUMBANI...PENALTI YA MORRISON YATEMBEA JUU YA LANGO

VIGOGO, Yanga SC wamelazimishwa sare ya pili mfululizo nyumbani baada ya kumaliza dakika 90 bila kufungana na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Sare hiyo inawaongezea pointi moja Yanga SC na kufikisha pointi 39 katika mchezo wake wa 20 wa msimu, ikibaki nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC yenye pointi 44 na mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 56 baada ya wote kucheza mechi 22.

Hiyo inakuwa sare ya pili mfululizo nyumbani baada ya Yanga kulazimishwa sare nyingine ya 1-1 na Mbeya City kwenye mchezo uliopita hapa hapa Dar es Salaam. 

Hata hivyo, Yanga itabidi wajilaumu wenyewe kwa kupoteza nafasi nzuri ya kupata bao dakika ya 73 leo baada ya kiungo wake Mghana, Bernard Morrison penalti kufuatia kupiga juu ya lango.

Penalti hiyo ilitolewa baada ya yeye mwenyewe, Morrison kuangushwa kwenye boksi na kipa wa Tanzania Prisons, Jeremiah Kisubi, ingawa refa Hance Mabena ilibidi akajiridhishe kwa msaidizi wake namba moja, Leonard Mkumbo kabla ya kutenga tuta

No comments