WATANZANIA WALIOPO WUHAN WAPO SALAMA-MAJALIWA
Mwambawahabari
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa
Mtume Muhammad S.A.W , Mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam,
Februari 16, 2020. Wa pili kushoto ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Zuberi Bin Ally (kulia) wakati aliposhiriki katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad S.A.W. , Mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam, Februari 16, 2020. Wa pili kulia ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam, Al Hadi Musa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Zuberi Bin Ally (kulia) wakati aliposhiriki katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad S.A.W. , Mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam, Februari 16, 2020. Wa pili kulia ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam, Al Hadi Musa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
......................................
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema vijana wa Tanzania wapatao 497 wanaosoma
katika vyuo mbalimbali vilivyoko kwenye mji wa Wuhan nchini China wote
wapo salama.
Kwa
sasa Mji wa Wuhan umewekewa zuio hakuna mtu anayeruhusiwa kutoka wala
kuingia, lengo likiwa ni kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi hivyo.
Mlipuko wa virusi vya corona ulianzia katika mji wa Wuhan.
Ametoa
kauli hiyo leo (Jumapili, Februari 16, 2020) kwenye Kumbukumbu ya
Mazazi ya Mtume Muhammad Swalla Allahu Alayh Wasallam iliyoandaliwa na
Nida Textile Mills (T) ltd, na kufanyika katika mtaa wa Indira Ghandi
jijini Dar-es-Salaam. Watu zaidi ya 1,500 wamefariki dunia kutokana na
mlipuko wa virusi hivyo.
Waziri
Mkuu amesema kutokana na zuio hilo wakazi wote wa mji huo wakiwemo
vijana wa Kitanzania wanapata huduma mbalimbali kupitia njia ya mtandao
ukiwemo ununuzi wa bidhaa mbalimbali.
“…Hakuna
usafiri hata wa umma unaofanya shughuli za kusafirisha watu katika mji
wa Wuhan kila mmoja anaetakiwa abakie katika makazi yake na kwamba
Serikali ya China na uongozi wa vyuo unawatunza wanafunzi wote wakiwemo
na Watanzania.”
Waziri
Mkuu amesema kwamba kwa sasa Wachina wameimarisha utoaji huduma kwa
njia ya mtandao hata kama mtu anataka kununua kitu ananunua kwa njia ya
mtandao. “Kama kijana ameishiwa basi atumiwe fedha kwa njia ya mtandao
ili aweze kujikimu wakati huu wa zuio.”
Waziri
Mkuu amesema jambo la muhimu kwa sasa ni usalama wao na kujali
maelekezo yaliyotolewa na Serikali ya China juu ya usalama wao pamoja na
wananchi wengine walioko katika eneo hilo.
Amesema
Serikali imeweka mitambo ya kupima watu katika maeneo yote ya mipaka na
kwamba inawataka wananchi washirikiane nayo katika kuhakikisha watu
wote wanaoingia nchini wanapita kwenye njia sahihi.
Pia,
Waziri Mkuu amerua kuwataka Watanzania waendelee kuwa watulivu na
kuitegemea Serikali katika kupata taarifa za mara kwa mara kuhusu
masuala mbalimbali zikiwemo na ya mlipuko wa virusi hivyo.

Post a Comment