Ads

OLE NASHA ATAKA WADAU SEKTA YA UTALII KUSHIRIKIANA

Mwambawahabari
NA Maria Kaira,Mwambawahabari

NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha, amezitaka Taasisi za mafunzo na wadau wa sekta ya Utalii  kufanya kazi kwa weledi pamoja ili kutatua changamto zilizopo ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020.

Akizungumza na wadau hao  jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga Kongamano la Kimataifa la kuunganisha wanataaluma na wadau wa sekta ya Utalii na Ukarimu ambapo amesema kama taifa ni lazima kuwekeza katika utayarisha wa vijana wakitanzania  ili kupata nguvu kazi yenye weledi na umahili wa kutosha  katika sekta ya utalii.

Ole Nasha  amesema kumekuwepo na ushindani mkubwa katika soko kutokana na  kuongezeka kwa wataalamu hao hivyo kunahitajika maandalizi mazuri ya rasilimali watu ili kuweza kushindana katika soko la dunia.

“Sekta ya Utalii ni moja ya Sekta inayoipatia Taifa fedha za kigeni kutokana na utalii hivyo  kukiwa na nguvu kazi yenye weledi na ufanisi wa kutosha nchi itaneemeka kupitia utalii na taifa litakuwa la mfano”amesema.


Aidha amesema Tanzania ni nchi ya pekee iliyojaliwa kuwa na rasilimali nyingi, nchi jirani zimepiga hatua kwenye kuvutia watalii sio kwamba wana vivutio vingi kuliko sisi ni kutokana na mambo mengine kuwa na nguvu kazi yenye weledi ndio maana kama Taifa tunawekeza katika kutayarisha vijana ili kuwa na nguvu kazi yenye weledi katika sekta ya utalii,” alisema na kuongeza.
.
Hata hivyo amevipongeza chuo cha Taifa cha Utalii na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuandaa mkutano wa kuwaunganisha wakufunzi na watoe huduma hiyo walio katika biashara ya Utalii kwani kwa pamoja wanaweza kutatua changamoto zilizopo.


Naye Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dkt. Shogo Mlozi amesema kwa kushirikiana na vyuo vingine vinavyotoa mafunzo ya utalii wataendelea kuimarisha mpango wa utoaji mafunzo kwa kufanya kazi karibu na watoa huduma ili kupata nguvu kazi yenye weledi na ujuzi.

No comments