Ads

Muhimbili-Upanga yanyakua makombe 2, Mloganzila yajipatia 1


Na Sophia Mtakasimba

Timu ya Hospitali ya Taifa Muhimbili –Mloganzila
imeinyuka Timu ya soka ya Muhimbili-Upanga mabao 3-1
wakati timu ya mpira wa pete ya Muhimbili-Upanga
imeichabanga Muhimbili-Mloganzila mabao 16- 11 katika
Bonanza la michezo lililofanyika Viwanaha vya JMK PARK
jijini Dar es Salaam.



Mchezo huu ulionekana kuwa na upinzani mkubwa huku
Muhimbili-Upanga wakionyesha kandanda safi na kujipatia
bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza.



Baada ya wachezaji wa Muhimbili-Mloganzila kupachikwa
bao walikuja juu na kulishambulia lango la Muhimbili-
Upanga na kujikuta wakijifunga na hivyo na mabao kuwa
1-1 katika kipindi cha kwanza.



Katika kipindi cha pili kila timu ilionyesha kukamiana huku,
Muhimbili-Upanga ikiishambulia kwa kasi timu ya
Muhimbili-Mloganzila, lakini bahati haikuwa yao kwani
walionekana kukosa nafasi nyingi za wazi.



Muhimbili-Mloganzila zikiwa zimebaki dakika 10
kumalizika kwa mchezo, ilibadilisha upepo kuwacharaza
wapinzani wao mabao mawili ndani ya muda huo na hivyo
ubao wa matangazo kusomeka mabao 3-1.



Bao la timu ya Muhimbili-Upanga lilipachikwa wavuni
kupitia mshambuliaji wake hatari, Abdalah Laiser wakati
mabao ya Muhimbili-Mloganzila yalifungwa na Abdul
Hamad, Omary Koppy na bao la tatu lilipachikwa wavuni
na Steven Wiligis.



Katika hatua nyingine, timu ya Kamba ya Hospitali ya
Taifa Muhimbili-Upanga ya wanaume na wanawake kila
moja wameshinda mabao 2-0 dhidi ya timu ya Kamba ya
wanaume na wanawake ya Muhimbili-Mloganzila.



Baada ya kupatikana kwa ushindi huu, mashabiki wa
Muhimbili-Upanga waliinuka kwenye viti na kuanza
kushangilia ushindi huu huku wakisema ‘wameicharaza
timu Muhimbili-Mloganzila hivyo waende kujifunza mchezo
wa kuvuta Kamba.’



Akizungumza baada ya michuoano hiyo, Mkurugenzi wa
Huduma za Tiba wa Muhimbili-Upanga, Dkt. Hedwiga
Swai amewashukuru watumishi kwa kujitoa katika
michezo kwani lengo si kutafuta ushindi bali kudumisha
uhusiano na upande uliopo kati ya Muhimbili-Upanga na
Muhimbili-Mloganzila.

No comments