Ads

TAKUKURU MKOA WA KINONDONI IMEWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA WATATU KWA MAKOSA YA RUSHWA

Mwambawahabari
                               Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni, Bi.Theresia Mnjagira akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es Salaam
                      ************************************
Maria Kaira, Mwambawahabari

 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni leo imewafikisha mahakamani watuhumiwa watatu wa manispaa hiyo kwa makosa tofauti ya kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu Cha 15(1)a na (2) Cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na rushwa namba 11/2007. 

 Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni, Bi.Theresia Mnjagira amesema kuwa January 6 mwaka huu Elgidius Kamugisha miaka (23) mkazi wa Kimara Baruti karani wa ushuru wa masoko manispaa ya Kinondoni aliomba rushwa ya sh.300,000/= na kupokea kiasi Cha sh 205,000/= kutoka kwa mfanyabiashara wa soko la makumbusho ili aweze kumsaidia asisumbuliwe na mpangaji wa awali wa kibanda Cha biashara kinachomilikiwa na manispaa ya Kinondoni. 


 Bi.Theresia amesema katika tukio la pili January 5,2020 mtuhumiwa Judith Ngoma miaka (39) mkazi wa Mabwepande na Afisa Mtendaji wa mtaa wa Maputo Mbweni Jijini Dar es salaam,aliomba rushwa ya sh.500,000/=na kupokea kiasi Cha sh. 280,000/= kutoka kwa mwananchi aliyehitaji kibali cha ujezi.


Amesema tukio la tatu mtuhumiwa Desdery Labury miaka (37) mkazi wa Tegeta ambaye ni mhandisi wa manispaa ya kinondoni January 21 mwaka huu aliomba rushwa ya sh. 1,000,000/= kutoka kwa mwananchi ili aweze kumpunguzia kulipa faini ya sh. Milioni 2,880,000/= aliyotakiwa kulipa baada ya kujenga nyumba bila kuwa na kibali cha ujenzi. 

 "Watumishi wa umma nawasihi kuzingatia maadili ya utumishi wa umma mnapotoa huduma kwa wananchi,pia Wananchi mtambue wajibu na haki zenu hali itakayowasaidia kuondoa dhana kuwa bila rushwa hakuna huduma" amesema

 Hatahivyo. Bi. Theresia amesema Takukuru ya mkoa wa Kinondoni inaendelea kuwasihi wananchi wote kuunga mkono serikali ya awamu ya tano katika kutekeleza sera ya mapambano dhidi ya Rushwa, huku akiwasihi wananchi kushiriki katika mapambano ya rushwa kwa kutoa taarifa za viashiria vya rushwa katika ofisi za Takukuru

No comments