LUKUVI KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS JUMATATU IJAYO.
Mwambawahabari
Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi Jumatatu tarehe 17 Februari 2020 atakwenda
katika halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa ajili ya kurudisha umiliki wa
ekari 750 kwa manispaa hiyo kama ilivyoelekezwa na Rais Magufuli.
Rais John Pombe Magufuli
alitoa siku saba kuanzia jumanne iliyopita kwa Wizara ya Ardhi kurejesha miliki
ya eneo hilo kwa Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni kufuatia kufuta miliki ya
eneo hilo ili kuwa chini ya Serikali.
Uamuzi wa Lukuvi ni utekelezaji
wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli alilolitoa
jumanne wiki hii baada ya kuzindua jengo la Manispaa ya Kigamboni na lile la
Mkuu wa Wilaya hiyo yaliyoko eneo la Gezaulole jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwa njia ya
Mtandao leo tarehe 13 Februari 2020 akiwa Abu Dhabi, Falme za Kiarabu anakohudhuria
Kikao cha Mawaziri wa Afrika Kuhusu
Masuala ya Nyumba na Maendeleo ya Miji Lukuvi alisema, jumatatu atakuwa ofisi
za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa ajili ya kutekeleza
agizo la Rais kuhusiana na urejeshaji miliki ya ardhi kwa halmashauri hiyo.
‘’Jumatatu tarehe 17 Februari
2020 saa tano asubuhi nitakuwa ofisi za Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni kwa
ajili ya kutekeleza agizo la mhe Rais la kukabidhi ardhi ambayo iko katika eneo
la Kigamboni’’ alisema Lukuvi
Kwa mujibu wa Rais
Magufuli, pamoja na kufuta umiliki wa eneo hilo ili kuwa chini ya Serikali lakini umiliki wake haujarerejeshwa katika Manispaa
ya Kigamboni na kutaka miliki hiyo kurejeshwa ndani ya wiki moja ili wananchi
wapange wanavyotaka.
Hata hivyo, Magufuli
alitahadharisha ardhi hiyo isije ikatumika vibaya kwani si ya viongozi bali ni
kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa kigamboni.
Post a Comment