DC MJEMA ALISHUKURU KANISA KWA MAOMBI YA KUIOMBEA NCHI NA UCHAGUZI MKUU
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Sophia Mjema akizungumza na waumini wa kanisa la TAG Aman Christian Centre Tabata
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Sophia Mjema akizungumza na waumini wa kanisa la TAG Aman Christian Centre Tabata ,hawapo pichani, mwingine ni Askofu wa kanisa hilo Laurence Kameta.
Na John Luhende
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Sophia Mjema amelishukuru kanisa la TAG Aman Christian Centre Tabata , kwa kuendesha maombi ya kufunga kuiombea nchi kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu.
DC Mjema ametoashukrani hizo kanisani hapo alipokuwa mgeni mwalikwa akiwakilisha Serikali katika maombi hayo maalumu ambapo alitumia nafasi hiyo kuwataka waumini wadini zote kufuata mfanono mwema wa kanisa hilo kwa kumuombea Rais pamoja na viongozi wengine waandamizi wa serikali katika majukumu yao yao uongozi ili waweze kumtanguliza Mungu mbele.
''Nawashukuru sana waumini na Baba askofu Kameta kwa kutenga muda wenu kuombea serikali na uchaguzi mkuu mzidi kubarikiwa na nitafikisha salaamu zenu kwa mhe.Rais Dkt John Pombe Magufuli kuwa mnamwombea ''Alisema .
Aidha aliwataka wanawake wa kanisa hilo kuchangamkia fursa za mikopo ya akinamama inayotolewa na Halmashauri ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Awali akimkaribisha mkuu wa Wilaya Askofu wa kanisa hilo Laurence Kameta alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kuleta nidhamu ya utumishi serikalini na kuendelea kudumisha amani na uhuru wa kuabudu.
''Nikushukuru sana pia wewe Mkuu wa Wilaya umekuwa kiongozi bora usiye bagua , unasikiliza wananchi wako nakumbuka siku ulikuja Tabata kusikiliza kero za wananchi ulikaa mpaka muda wa saambili usiku hadi ulipo msikiliza kilamtu aliye kuwa na kero, Mungu akubariki sana ,tufikishie salamu zetu kwa Rais sisi tunafanya kazi , hapa kila Muumini anakazi ya kufanya hakuna aliyekaatu bila kujishughulisha najua Rais anasisitiza watu kufanya kazi''Alisema
Akitoa neno kabla ya kuanza kwa maombi Rev Annael Gttlob Pallangyo alisema Mungu ana agenda na Tanzania na wanamwomba Mungu ili katika uchaguzi wa mwaka huu wachaguliwe viongozi watakao beba agenda ya Mungu watao mtanguliza Mungu mbele katika utumishi wao.
Post a Comment