Ads

BALOZI WA UFARANSA NCHINI TANZANIA AHIMIZA UTUNZAJI VYANZO VYA MAJI ZIWA VICTORIA


Ubalozi wa ufaransa nchini Tanzania umewakutanisha wadau mbalimbali kujadili ni namna gani nchi zinazonufaika na ziwa victoria zitakavyoweza kulinusuru ziwa hilo na shughuli za kibinadamu ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa uchafuzi  na uharibifu wa vyanzo vya maji katika ziwa hilo.

Akizungumza wakati akifungua mjadala huo uliofanyika jijini Dar es salaam balozi wa Ufaransa hapa nchini Frederic Clavier amesema  Ufaransa imechukua hatua mbalimbali kusaidia wakulima katika nchi zinazonufaika Moja kwa moja na ziwa Victoria kuondokana na matumizi ya kemikali katika kilimo ili maji yanayoingia katika ziwa  yasiathiri viumbe waliomo katika ziwa na kuharibu vyanzo vya maji vya ziwa hilo

 "tunafanya mjadala huu kwa mara ya pili hapa Tanzania Kama  mnavyoona hapa pia tumewashirikisha wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam na wale wa chuo cha sayansi shirikishi cha Muhas na wataalamu mbalimbali na hakika serikali ya ufaransa imeshiriki kikamilifu katika suala la ziwa victoria  na jinsi ya kulitunza ziwa hilo kwa nchi nufaika hivyo  ufaransa tumeamua kutoa  Dola milioni moja za kimarekani kwa Tanzania, Agro ecology ambazo zitawasaidia wakulima wadogo wanaoendesha shughuli za kilimo kuzunguka ziwa maana yake kufanya kilimo cha kisasa kwa kupunguza matumizi ya kemikali, bidhaa za kemikali ambayo yanaathiri ziwa hilo kwa wakulima" alisema Clavier

Aidha balozi huyo wa ufaransa hapa nchini aliongeza kuwa shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya Maji ya Ziwa victoria katika nchi zinazolizunguka ziwa hilo kumechangia kuongezeka kwa uchafuzi wa maji, hali inayosababisha kupungua kwa idadi ya Samaki na viumbe hai wengine wanaopatikana katika ziwa hilo.

Naye mkurugenzi wa bodi ya maji ya ziwa Victoria Florence Mahay alisema nchi za Uganda ,Kenya na Tanzania ni wanufaika wa moja kwa moja wa ziwa hilo, lakini suala la uchafuzi katika vyanzo vya maji yanayoingia katika ziwa hilo ni changamoto, hivyo wao Kama bodi ya maji wamefanya jitihada za kutunza vyanzo vya maji hayo ikiwa ni pamoja na kuunda kamati maalum za zinazohusisha wananchi wanaolizunguka ziwa sambama na kutoa elimu jinsi
shughuli za kibianadamu zinavyoweza kuathiri viumbe hai vilivyomo katika ziwa hilo ikiwa ni pamoja na samaki na kuahidi kuwa kupitia mradi wa kupunguza uharibifu wa ziwa hilo ambao pia Ufaransa imetoa fedha za kufadhili wataendelea kutoa elimu juu ya athari za kuliharibu ziwa hilo

Kwa upande wake Mtafiti wa Ekolojia ya maji baridi na Mdhadhiri kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam Dkt Lulu Kaaya alisema hali ni mbaya kutokana na kemikali sambamba na mabadiliko ya tabia nchi kuathiri samaki na viumbe wengine waliomo katika ziwa hilo hivyo Kama hazitatumika jitihada kulinusuru hali itakuwa mbaya zaidi.

Mjadala huo uliopewa jina la "the night of ideas" unaoratibiwa na ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania umekuwa chachu ya mabadiliko hasa katika nchi za Kenya,Uganda na Tanzania katika kulinda vyanzo vya maji vya ziwa Victoria na uhifadhi  wake ambapo Tanzania hufaidi zaidi ya asilimia 51 ya ziwa hilo.

No comments