Baada ya kibano waamuzi kuibeba Simba, Mabingwa hao wameanza kuonja jito ya jiwe.

Na Mwandishi Wetu Dar
Kufuatia baadhi ya waamuzi kupewa onyo na wengine kufungiwa wakidaiwa kuibeba kupata ushindi clabu ya Simba , Mabingwa hao wameanza kuonja joto ya jiwe ambapo leo mchezo ulichezeshwa kwa kuzingatia sheria za socer wamejikuta wakilala 1-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
JKT Tanzania inayofundishwa na kocha bora wa Ligi Kuu msimu wa 2017-2018, Abdallah Mohammed ‘Baresi’, inafikisha pointi 30 baada ya kucheza mechi 20, ingawa inabaki nafasi ya nne.
Kwa Simba SC Simba SC iliyo chini ya kocha Mbelgiji, Sven Ludwig Vandonbroeck anayesaidiwa na mzalendo, Suleiman Matola, kocha wa makipa Muharami Mohamed ‘Shilton’ na kocha wa Fiziki, Mtunisia, Adel Zrane inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 50 za mechi 20 sasa, ikiwazidi pointi 12 Azam FC wanaofuatia.
Bao la kuiliza Simba SC limefungwa na nyota tegemeo Adam Adam kwa kichwa dakika ya 24 akimalizia krosi ya beki Damas Makwaya.
JKT Tanzania walicheza kwa nidhamu kubwa leo, wakiwabana wachezaji wa Simba na kuwatibulia mipango yao yote ambao wamezoea huruma za waamuzi.
Dakika ya 51 mshika kibendera namba mbili Kassim Mpaga wa Dar es Salaam alimnyooshea kibendera cha kuotea kiungo Mbrazil wa Simba, Gerson Fraga ‘Viera’ wakati anamalizia kwa kichwa mpira wa juu wa kiungo Mkenya, Francis Kahata, ingawa hakuwa amezidi.
JKT Tanzania walipata pigo dakika ya 77 baada ya kipa wao, Patrick Muntary kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Abdulrahman Mohamed ‘Wawesha’ aliyekwenda kumalizia vizuri.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Benno Kakolanya, Haruna Shamte, Gardiel Michael, Kennedy Juma, Pascal Wawa, Gerson Fraga ‘Viera’/Clotous Chama dk63, Luis Miquissone, Jonas Mkude, Meddie Kagere, Ibrahim Ajibu/John Bocco dk63 na Shiza Kichuya/Fransis Kahata dk46.
JKT Tanzania; Patrick Muntary/Abdulrahman Mohamed dk78, Michael Aidan, Edward Songo, Edson Katanga, Damas Makwaya, Nurdn Mohamed, Mwinyi Kazimoto, Hafidh Mussa/Kelvin Nashon dk62, Mgandila Shaaban, Daniel Lyanga/Mussa Said dk90 na Adam Adam.
Post a Comment