Wafanyabiashara wapewa somo kutumia mfumo wa utoaji taarifa.
WAFANYA biashara nchini wamehimizwa kutumia Mfumo wa Utoaji Taarifa za Kibiashara uliomo kwenye Dirisha la Taifa la biashara (the Tanzania National Business Portal) ili kuweza kufahamu taratibu za usafirishaji nje ya nchi, uingizaji nchini na upitishaji wa mazao na bidhaa mbalimbali nchini.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Leseni wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Andrew Mkapa, alipokua akizungumza katika mahojiano maalumu.
Mtu anapoingia kwenye Mfumo huo , kule anaweza kuona taarifa za hatua kwa hatua ambazo mfanyabiashara anapaswa kuzipitia na kuzifuata ili kupata leseni na vibali vinavyohitajika toka Taasisi mbalimbali ili aweze kusafirisha nje ya nchi, kuingiza na au kupitisha nchini bidhaa na mazao mbalimbali ,alisema Bw. Andrew.
Bw. Andrew alisema kwa mfano Tanzania wameishaweka taarifa hizo zinazohusiana na usafirishaji nje ya nchi wa mazao makuu ya kimkakati kama vile, Kahawa, Karafuu, Korosho, chai na mengine ambapo zinazohusiana na uingizaji nchini wa Madawa, Vipodozi, Vifaa tiba, Magari na vinginevyo.
Aidha alisema sasa mfanyabiashara akiingia kwenye huo mfumo anaweza kuona ni hatua gani na ngapi anapaswa kupitia, vibali au leseni gani anatakiwa awe navyo ili aweze ama kusafirisha nje ya nchi, kuingiza ndani au kupitisha nchini bidhaa hizo.
Aidha alifafanua kuwa lengo la kuweka mfumo huu ni kumsaidia mfanyabiashara aweze kuwa na taarifa za kutosha kabla ya kuanza kufanya utaratibu wa ama kuuza bidhaa nje ya nchi, kupitisha au kuingiza nchini.
Pia alisema mfumo hou utasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha ufanyaji biashara hapa nchini lakini pia utarahisisha upatikanaji wa taarifa hizo kwa wafanyabiashara kutoka nchi nyingine ambao wangependa kufanya biashara hapa nchini.
“Uboreshaji wa mazingira ya biashara nchini ni pamoja na kupunguza muda, kupunguza gharama, lakini pia inapobidi kupunguza Sheria na Kanuni mbalimbali ambazo zinaonekana si za lazima sana na ni vikwazo katika ufanyaji biashara. Hivyo mfanyabiashara anapokua amezifahamu hizi taratibu kabla, zitamsaidia sana na kumpa nafasi ya kujiandaa kuzitekeleza bila kupoteza muda mwingi wa kuzunguka na kuzitafuta kwanza alisema Bw. Mkapa.
Katika hatua ya mwisho Bw. Mkapa ametoa wito kwa wafanyabiashara kutembelea Taarifa hizo kupitia ama tovuti ya BRELA yani www.brela.go.tz kisha kubonyeza katika mahali palipo andikwa ‘Trade Information Module ambapo mfumo utampeleka katika dirisha la taifa la biashara, au moja kwa moja kwenye Dirisha la biashara kwa anwani pepe ya www.business.go.tz .

Post a Comment