Ads

Mkuu wa JKT Brigedia Jenerali Charles Mbuge akutana na Makamanda kupanga Mikakati.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Charles Mbuge.

Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Charles Mbuge amewataka makamanda katika nafasi mbalimbali ndani ya jeshi hilo kutekeleza majukumu yao kwa vitendo pamoja na kujitathmini.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa kikao kazi kilichowakutanisha wakuu wa idara wakiwemo wakurugenzi kutoka Makao Makuu ya JKT, Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT), Makamanda wa vikosi, wakuu kanda za ujenzi pamoja na wakuu wa shule na Chuo, Mkuu wa JKT Brigedia Jenerali Charles Mbuge, amesema kuwa lengo la kikao ni kujadili utekelezaji wa majukumu ya JKT.

"Nashukuru kwa kunipongeza kuteuliwa kuwa mkuu wa JKT, kauli mbio yangu ni maneno sio kazi, kazi ni vitendo" amesema Brigedia Jenerali Mbuge.

Ameeleza kuwa ni vizuri kujipima na kujitathmini kila mmoja katika nafasi yake ili kuona kama inamtosha kulingana na mjukumu yake.

Brigedia Jenerali Mbuge amesema kuwa kupitia kikao kazi hicho wanatarajia kupata mrejesho wa utekelezaji wa majukumu, kupanga mipango pamoja na kupeana uzoefu katika utendaji kazi.

Amesema kuwa makamanda wa vikosi vizuri kuaendelea kuelimisha jamii kuhusu JKT haitoi ajira bali ipo kwa ajili kuwajenga vijana kuwa wazalendo.

"Katika mafunzo kwa vijana tusisitize upendo kushirikiana pamoja na nidhamu" amesema Brigedia Jenerali Mbuge.

Hata hivyo amefafanua kuwa kupitia kikao hicho wanatarajia kuangalia malenzi ya vijana baada ya kupata mafunzo, mikakati ya vijana kujiudumia wakiwa katika mafunzo, kuongeza idadi ya vijana katika mafunzo ya JKT.

Mkurugenzi wa Fedha wa JKT Kanali Hassan Mbena, amesema kuwa JKT inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi pamoja na kuweka mipango.

Amesema kuwa ili kuipunguzia serikali mizigo JKT inameaza kuzalisha mazao mbalimbali ikiwemo mpunga, mahindi pamoja na maharage kwa ajili ya kuwapatia vijana chakula ambao wapo katika mafunzo.

Kaimu Mkuu Tawi la Utawala JKT Kanali Julius Kadawi, amesema kuwa kupitia kikao kazi watapata dira katika utekelezaji  wa masuala mbalimbali katika kuleta tija.

Amesema kuwa tumefanikiwa kufungua  kambi kikosi namba 830 kibiti katika wilaya ya Pwani ikiwa ni sehemu ya kuongeza idadi ya vijana wanaopata mafunzo JKT.

Katika kikao hicho watajadili kuwa muda siku mbili kuanzia leo Oktoba 23 hadi 24 mwaka huu ambapo ni mara ya kwanza Mkuu wa JKT Brigedia Jenerali Charles Mbunge kukutana na wakurugenzi pamoja na watendaji ili kubadilishana uzoefu na kupanga mikakati ya utekelezaji.

No comments