Akizungumza
na wanahabari katika kambi hiyo iliyopo katikati ya Jiji la Dar es
Salaam alisema jumuiya hiyo imefanya jambo jema la kujitolea kutoa tiba
bure na dawa na kubainisha kuwa taasisi zingine zinatakiwa kuiga mfano
kwa kutoa huduma za afya bure.
“
Leo nafanya ziara ya kutembelea kambi ya Khoja Shia nawapongeza kwa
huduma ya afya ya bure wanayoitoa kwa wananchi nawaomba wananchi
wachangamkie fursa hii waje kwa wingi,” alisema Meya Kumbilamoto.
Alibainisha
kuwa mara ya kwanza walikuwa na mpango wa kuipatia jumuiya hiyo eneo la
Viwanja vya Mnazi Mmoja wakijua kwamba wananchi watakuwa wengi lakini
imekuwa tofauti kwani eneo la kambi ni kubwa linatosha.
Alisisitiza
kuwa wananchi wanatakiwa kufika kambini kupatiwa vipimo vya macho
ikiwemo presha ya macho na mtoto wa jicho pamoja na huduma ya meno.
Kwa
upande wake Mratibu wa kambi hiyo, Ali Bandali alisema huduma za
matibabu ya macho na meno bure na kwamba madhumuni yake ni kujenga taifa
la wananchi wenye afya njema.
Bandali
alisema kambi ya vipimo na matibabu bure hutolewa kila jumamosi na
jumapili na kwamba watu 700 wameshafikiwa kati yao 50 wamekutwa na
matatizo ya mtoto wa jicho yanayohitaji kusafishwa na kufanyiwa
upasuaji.
Naye
Mwanajumuiya hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Kata
ya Kisutu, Mahmood Walji aliishukuru na kuwapongeza madaktari kwa
huduma wanayotoa na kuwataka wananchi wajitokeze
Mtalaam
wa Macho wa kambi hiyo, Roby Samwel alisema mwitikio wa wananchi ni
mzuri huku akibainisha watu 50 wamekutwa na tatizo la mtoto wa jicho na
kuwahimiza wananchi kwenda kupatiwa vipimo na matibabu ya bure.
Post a Comment