Meya Kumbilamoto ahimiza vijana kushiriki michezo.
Mwambawahabari
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza na vijana wa Timu ya Mpira Vingunguti leo asubuhi.
Kumbilamoto ametumia nafasi hiyo kuwashukuru Vijana hao na wananchi wa Ilala kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha katika Daftari la wapigakura kwaajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019.
"Michezo ni Afya,Udugu,na pia niajira nahimiza Vijana tupende michezo natuendelee kushirikiana nami nitakuwa nanyi bega kwa bega" Alisema Kumbilamoto.
Pia amewakabidhi mpira na kuwataka vijana hao wazidi kumuombea dua Rais Magufuri kwa kazi kubwa anayoifanya yakujenga nchi.
Akishukuru kwa niaba ya wachezaji kiongozi wa Timu hiyo amemshukuru Meya kwa kuwatembelea nakuwapa Mpira na kusema kuwa kabla ya mpira huo walikuwa wakikodi kwa Mtu.
Post a Comment