Kumbukizi miaka 20 baba wa Taifa kufanyika Dar Oktoba 8-14
Watanzania pamoja na wadau mbalimbali wametakiwa kushiriki kikamilifu katika kumbukizi za baba wa Taifa miaka 20 linalotarajiwa kufanyika kuanzia October 8-14 mwaka huu katika uwanja wa uhuru jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Mjukuu wa baba wa Taifa Mwalimu Nyerere Magori Sophia, amesema kuwa baada ya kuendelea kutafakari mchango wa kama wajukuu wameona kuonyesha dhamira ya kufanya kumbukizi pamoja na kuwakaribisha wazalendo wanaompenda na kuheshimu mchango wa baba wa Taifa.
Bi Sophia amesema kuwa ni vyema wadau wakiwemo makampuni na taasisi mbalimbali kushiriki kwa kuonyesha dhamira ya kufanya kumbukizi.
"Baba wa Taifa alikuwa baba wa Afrika haitakiwi kusahau mchango wake na hakuna nchi au Taifa lingine linaloweza kuenzi michango wake kwa taifa lets" amesema Bi Sophia.
Hata hivyo ametoa wito kwa Taasis, Makampuni kuwa walezi, washauri, wahisani, wafadhili katika kuwashika mkono na kufanikisha kumbukizi hiyo kuwa endelevu.
Kumbukizi hiyo imebeba mikakati mbalimbali kama kujitambua, Kuchangia damu, kutunza mazingira, uzalendo kwa vitendo pamoja na pendekezo la mtaala wa uzalendo.
"Kumbukizi la babu yangu sio fursa kwa mtu yoyote kujipatia faida binafsi kwa baadhi ya watu wachache wanavyoweza kufikiria"
Bi. Sophia amewashukuru wanakamati kwa ushirikiano wao katika kuhakikisha wanafanikisha kumbukizi hilo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Elias Tarimo, amesema kuwa uzalendo ni nguzo muhimu katika kufanya kazi ili tuweze kuishi maisha yetu katika kuleta ufanisi kwa vitendo.
Amesema kuwa ni vizuri vijana kushiriki ili kuwa na moyo wa kizalendo katika kujenga taifa letu.
"Siku hiyo kutakuwa na vikundi tmbalimbali vya sanaa ambavyo vitaonyesha mchango wako" amesema Bw. Tarimo.
Post a Comment