HESLB YATANGAZA WANAFUNZI WALIOPATA MIKOPO ELIMU YA JUU 2019/2020
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Abdul-Razaq Badru akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya awamu ya kwanza yenye wanafunzi 30,675 wa mwaka wa kwanza wa masomo 2019/2020 waliofanikiwa kupata mikopo yenye thamani ya shillingi bilioni 113.5.
Akizungumza na waandishi waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Bw. Abdul-Razaq Badru, amesema kuwa katika awamu ya kwanza wanaume ni 19,632 sawa na asilimia 64, wanawake wakiwa 11,043 sawa na asilimia 36.
Bw. Badru, amesema kuwa serikali imetenga shillingi bilioni 450 zinazolenga kuwanufaisha jumla ya wanafunzi 128,285 kati yao wanafunzi 45,000 ni mwaka wa kwanza na wengine 83,285 ambao wanaendelea na masomo.
Amefafanua kuwa ili muombaji aweze kujua kama amepangiwa mkopo anapaswa kuangalia akaunti zao binafsi (SIPA- Student's Individual Permanent Account) walizofungua wakati wanaomba mkopo kupitia mfumo wa HESLB (olas.heslb.go.tz).
"Tunaanza kupeleka fedha vyuoni kesho kuwa kuwa serikali imeshatukabidhi shillingi bilioni 12p5 ambazo tuliomba kwa ajili ya malipo kati ya Oktoba hadi Disemba " amesema Bw. Badru.
Ameeleza kuwa orodha ya awamu ya pili ya wanafunzi waliopata mikopo inatarajia kutangazwa kabla ya Oktoba 25 mwaka huu baada kukamilisha kwa uchambuzi wa maombi ya mikopo kutoka kwa wanafunzi waliochelewa kukamilisha taratibu za udhahili.
Hata hivyo amefafanua kuwa ugawaji wa mikopo imezingatia makundi maalum yenye uhitaji, ambapo katika awamu ya kwanza wanafunzi 6,142 yatima, wenye ulemavu 280 pamoja na wengine 277 wanatoka katika familia zinazofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Post a Comment