Ads

Waziri Kamwelwe azindua TMA, Sasa rasmi kuwa Mamlaka.


Na Noel Rukanuga Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandishi Isack Kamwelwe ameipongeza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kufanya kazi kwa ufanisi jambo ambalo itasaidia taifa kuendelea kupiga hatua katika nyanja mbalimbali ya kimaendeleo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa TMA, Mhe. Kamwelwe, amesema kuwa TMA imekuwa ikifanya kazi zake kwa ufanisi mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yake.

Katika kipindi chote imekuwa ikifanya kazi kama Wakala, kuanzia leo imepandishwa na kuwa Mamlaka na kuweka historia katika taifa hili.

"Kazi ya TMA ni muhimu kwa taifa katika kupiga hatua kimaendeleo, naipongeza TMA kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya" amesema Mhe. Kamwelwe.

Hata hivyo ameipongeza bodi ambayo imemaliza muda wake leo kwa utendaji wao kwa kuhakikisha wamefanikisha kuisaidia katika utendaji.

Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)Dkt. Agnes Kijazi, amesema kuwa kuzinduliwa kwa TMA ni muendelezo kazi nzuri wanayofanya.

Dkt. kijazi amesema kuwa tangu mwaka 1999 walikuwa wakitekeleza majukumu yao kama wakala, lakini kuanzia sasa tumekuwa Mamlaka kwa mujibu wa sheria.

"Tumekuwa tukiongezeka kwa viwango vya utabiri kutoka asilimia 75 hadi kufikia asilimia 87-90" amesema Dkt. kijazi.

Katika hatua nyengine ameeleza kuwa TMA imefanikiwa kuwa na vituo viwili vya data ambavyo vipo Mkoa wa Songea na Bukoba.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji-Zanzibar Bw. Mustafa Jumbe, amesema kuwa taarifa ya hali ya hewa ni muhimu kutokana serikali ya zanzibar imekuwa ikichukua hatua.

Bw.Jumbe amesema kuwa taarifa za TMA ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku katika kutupa muongozo kuhusu hali ya hewa.

"Zanzibar  itaendelea kutoa ushirikiano kwa TMA ili kuendelea kufanya kazi zake kwa ubora" amesema Bw. Jumbe.

No comments