Ads

JPM AMTUMBUA MKUU WA MKOA MOROGORO.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Ijumaa Septemba 20,2019 amefanya Mabadiliko na Kuteua Viongozi wengine katika baadhi ya nafasi mbalimbali katika Serikali. 

Uteuzi umetangazwa  na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. John Kijazi. 

Rais Magufuli amemteua Loata Sanare ambaye ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha kuwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro,nafasi ambayo ilikuwa inashikiliwa na Stephen Kebwe ambaye uteuzi wake umeteguliwa.. 

Aidha Rais Magufuli amemteua Musa Masele ambaye alikuwa msaidizi wa mkuu wa mkoa wa Geita, kuwa mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Mkoani Morogoro.

Mbali na teuzi hizo pia Rais amefanya mabadiliko ambapo, Mkuu wa Wilaya ya Tarime Charles Kabeho, amehamishiwa wilaya ya Chato na Mkuu wa Wilaya ya Chato Msafiri Mtemi amehamishiwa Wilaya ya Tarime. 


Aidha, Rais Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi 12 watakaowakilisha Tanzania nchi mbalimbali, katika uteuzi huo wamo pia Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Dk Modestus Kipilimba

No comments