RC MAKONDA KUWASILISHA MUSWADA WA MAPENDEKEZO YA MABADILIKO YA SHERIA YA MIRATHI KWA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* anatarajia kuwasilisha *Muswada wa mapendekezo ya Mabadiliko ya Sheria ya Mirathi* na Sheria ya Ndoa kwa *Waziri wa Katiba na Sheria* ili ziweze kufanyiwa *marekebisho* kutokana na Sheria hizo *kupitwa na wakati* na kuonekana kuwa *kandamizi kwa wanawake* pindi Mume anapofariki jambo linalopelekea *Mateso na Manyanyaso kwa Wajane.*
*RC Makonda* amesema miongoni mwa *Sheria kandamizi* zinazotakiwa kufanyiwa mabadiliko ni Sheria ya Kiserikali ya *Mirathi ya Mwaka1865,* Sheria ya Mirathi ya *Kimila ya Mwaka1963* na Sheria ya Mirathi ya *Kidini ya Mwaka1963* ambazo kimsingi zimeonekana kuwa na *Mapungufu makubwa* na zimepitwa na wakati.
RC Makonda* amevitaja vipengele anavyopendekeza kufanyiwa maboresho ni pamoja na *kumpa uhalali Mke wa marehemu kushiriki katika vikao vya mgawanyo wa mali,* mjane kupewa *haki ya kurithi na kusimamia mali za marehemu*, Mjane *kutoondolewa kwenye nyumba* wala Mali kuhamishwa, *Usawa wa watoto katika kumiliki mali* za marehemu bila kujali jinsia pamoja *haki ya mtoto wa nje ya Ndoa kurithi Mali.*
Vifungu vingine ambavyo *RC Makonda* ameeleza kuwa ni kandambizi kwa Mjane ni pamoja na kile kinachoruhusu *Mjane kurithiwa* na kile kinachomnyima *Mwanamke haki ya kurithi ardhi ya ukoo.*
*RC Makonda* amesema chimbuko la hayo yote ni *Kongamano la Wajane zaidi ya 5,181* alilohitisha mwezi April ambapo katika kongamano hilo alipokea *Kero na Malalamiko* mbalimbali kutoka kwa Wajane jambo lililopelekea *kuunda kamati* iliyoshirikisha Wadau na Wataalamu mbalimbali kutoka *Serikalini na Asasi za Kiraia* waliopitia malalamiko hayo na kutoka na mapendekezo hayo.
Post a Comment