Ads

RC MAKONDA ATOA MWEZI MMOJA KWA MANISPAA YA KINONDONI KUANZA UJENZI WA FUKWE ZA COCO.




Mwamba wa habari
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo August 09 ametoa Mwezi Mmoja  kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuhakikisha ujenzi wa maboresho ya Fukwe za Coco unaanza mara moja na kama wakishindwa watanyang'anywa fedha hizo na kutafutwa mzabuni.

Mapema leo RC Makonda akiambatana na Katibu Tawala wa mkoa huo wamefika kwenye ufukwe huo kwaajili ya kuangalia maendeleo ya mradi lakini wameshangazwa kuona hakuna chochote kinachoendelea wakati tayari Rais Dkt.John Magufuli alishatoa kiasi cha Shilingi Bilioni 14 za ujenzi huo lakini fedha hizo zimebaki kwenye akaunti bila matumizi huku watendaji wakilumbana kwenye  vikao.

RC Makonda amesema kinachomsikitisha zaidi ni kuona mshauri wa mradi amebadili mchoro wa Mwonekano mpya wa fukwe ambao ndio ulioombewa fedha kiasi cha Bilioni 14 na kuja mchoro wake mwingine wa Shilingi bilioni 40  bila kujua fedha hizo zitatoka wapi jambo ambalo RC Makonda amelizungumzia kama mpango wa  hujuma kwa serikali.

Aidha  RC Makonda  amewataka  wananchi wajue kuwa kinachochelewesha mradi ni uzembe unaofanywa na watendaji wachache ambao wameishia kushinda kwenye vikao.


No comments