RC MAKONDA ATOA FURSA KWA WAFANYABIASHARA UCHORAJI , VINYAGO MKUTANO WA SADC
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda ametoa fursa kwa wasanii wa uchoraji na wachonga vinyago kufanya biashara katika Mkutano Jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kwa kuuza bidhaa zao.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na wasnii hao Mhe. Makonda amesema kuwa katika mkutano wa SADC unaotarajia kufanyika hivi karibuni hapa nchini kutakuwa na wageni zaidi ya I,OOO jambo ambalo ni fursa kwa kuuza vinyago kwa wageni na watanzania.
Amesema kuwa ni fursa kwa wasanii kuuza bidhaa za picha na vinyago kando ya barabara katika maeneo ya posta karibu na chuo cha IFM.
"Kuna barabara mbili zitafungwa ili muweze kufanya biashara, naomba viongozi wapange utaratibu mzuri ili kila mmoja apate nafasi ya kuuza bidhaa yake" amesema Mhe. Makonda.
Amesema kuwa kila mfanyabiashara atafanya biashara yake kwa muda wa siku I5 bila kutozwa gharama yoyote.
Mhe. Makonda ameeleza kuwa lengo ni kuhakikisha wafanyabiasha hao wanatumia fursa ya mkutano wa SADC kwa kupata kipato kizuri.
Post a Comment