RC Makonda ampongeza jpm
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amempongeza Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Nchi 16 zinazounda Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo amemtakia Utumishi mwema uliotukuka katika nafasi hiyo.
RC Makonda amemshukuru Rais Magufuli kwa kuweza kupigania hoja ya Lugha ya Kiswahili kuingia katika Lugha Nne zinazotumiwa katika Jumuiya ya SADC na kuwahimiza Walimu, Baraza la Kiswahili Tanzania na wataalamu wa kiswahili kuchukulia hatua hiyo kama fursa ya ajira.
RC Makonda amewataka Wafanyabiashara na wanachi kuchangamkia fursa za Kibiashara zinazopatikana katika nchi wanachama ikiwemo Fursa ya kuuza Vyakula na mazao.
Pamoja na hayo RC Makonda* amewashukuru Wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam* kwa ukarimu na utulivu walioonyesha kwa kipindi chote cha Ugeni wa SADC jambo lililowezesha Wageni Kuingia nchini salama na kuondoka salama.
Post a Comment