Ads

RC MAKONDA AKINUKISHA WANAUME WA DAR WALIOWAAHIDI WANAWAKE KUWAOWA NA KUWALAGHAI.


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amezungumzia mpango mkakati wa kushughulikia wanaume wanaowalaghai wanawake kwa kuwaahidi ndoa ikiwa ni Pamoja na kusajili ndoa zote Katika mkoa huo.

Rc Makonda ameyasema hayo Leo Agosti 12, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema wanaume wengi wa mkoa huo wamekuwa wakiwadanganya wanawake kuwaoa na badala yake kutokomea.

"Nimepokea malalamiko mengi sana kutoka kwa kina dada, Wakina dada wa Mkoa wa Dar Es Salaam wengi wamechoka kutapeliwa, Vijana na wanaume wamekuwa wakiwaahidi kuwaoa alafu wanaingia mitini, Na wamefanya watoto wengi wa kike wamekua na majeraha moyoni".- Paul Makonda, RC, Dsm

Amesema hawezi kuendelea kuona wakina Dada wengi wanakuwa na majeraha moyoni na kusema kuwa mpango kanzi data maalumu itakayoweza kusajili ndoa zote .

Aidha amesema mbali na mpango huo atatumia mkutano wa SADC unaendelea nchini Tanzania kupata uzoefu wa nchi nyingine wanafanya nini Katika kuondoa vitendo hivyo.

Mbali na hayo Rc Makonda amewapongeza wakazi ya jiji la Dar es Salaam kwa kuweza kuweka mazingira Safi ambapo amesema usafi huo unatakiwa uendelee zaidi kwani wiki hiindio ugeni unaanza kufika hapa nchi.

No comments