Ads

MEYA ILALA WAUMINI WAKIWEZESHWA KIUCHUMI SADAKA MAKANISANI ZITAONGEZEKA ,AWATAKA KUOMBA MIKOPO YA HALMASHAURI.



Na John Luhende 
Mwamba wa habari
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto , amewataka  wachungaji  kuwahamasisha  waumini  wa makanisa yao kujiunga katika vikundi  ili waweze kupatiwa mikopo isiyokuwa na  riba inayo tolewa na Halmashauri, na kumuombea Rais John Pombe  Magufuli kwa kazi kubwa  anayoifanya ya kuliongoza taifa  na  kuwezesha watoto wa masikini kupata elimu bure .

Meya Kumbilamoto ametoa kauli hiyo  katika kanisa la EAGT Vingunguti  alipokuwa akitoa sadaka ya shukrani  ambapo pia ametoa mifuko  20  ya saruji na mchanga roly moja  kwaajili ya  kumalizia ujenzi wa kanisa hilo na kusema kuwa njia pekee ya kuya saidia makanisa kupata sadaka nyingi ni kuwawezesha waumini kuwa na kipato.

‘’Mahali hapa  ni mahali sahini  mliniombea wakati nagombea  nami niliahidi kuwa nitamshukuru Mungu kwa kunifanikisha leo nime kuja na sadaka yangu ya shukrani  pamoja na  hilo pia mmenieleza kuwa mnataka kumalizia ujenzi wa kanisa mnahitaji mifuko 20  ya saruji  leo nina wapa mifuko 10 , niutapa tena mingine 10 mkitumia hii ikiisha pia ntamtuma katibu atawaletea mcha lory moja  ‘’Alisema

Aidha ame mshukuru rais  Magufuli kwa kutoa elimu bure na kusema kuwa kata ya vingunguti wananchi wake wengi ni masikini  kwa kuungamkono  elimu bure kwa kushirikia na na wadau mbalimbali wamefanikiwa kuinua kiwango cha ufauli kwa wanafunzi  kwa kutoa chakula kwa shule zote za kata hiyo.

Kwaupande wake Mchungaji  kiongozi wa  kanisa  la EAGT  upendo Vingunguti  Marttini Mhokole  pamoja na kushuru  meya kwa  msaada huo , amewataka watu wenye fedha  kuzitazama nyumba za ibada  kwani huko ndiko watu wanajengwa kiroho  na kufanya taifa kumcha  Mungu.

‘’Niviongozi wachache sana wanaokumbuka baada ya kufanikiwa tunamshukuru sana Meya  kwa msaada  huu  naomba na viongozi wengine  tusiache ktoa kwaajili ya nyumba za ibada   taifa hili linategemea kujengwa na wacha Mungu tusiliache likaharibika kwa kutokuwa na viongozi wasiokuwa na hofu ya Mungu’’Alisema

Wakati akitoa msaada huo  alitaka waumini  wasichangishwe kwaali ya ujenzi huo  kwakuwa yeye amemalizia , waumini  wa kanisa hilo wamepokeaje msaada huo wamepokea kwa shangwe msaada huo na kusema kuwa wataelekeza nguvu zao katika kufanya mambo mengine baada ya ujenzi huo kumalizika .



No comments