Maandalizi ya SADC Meya Kumbilamoto aingia mtaani kuhimiza usafi.
Mwambawahabari
Katika Kuhakikisha jiji la Dar es salaam lina kuwa na mandhali ya kupendeza hasa Manispaa ya Ilala ambayo ndiyo ina chukua nafasi kubwa ya katikati ya Jiji, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto, amefanya ziara kuhimiza usafi wa mazingira.
Akizungumza, katika ziara hiyo katika eneo la Serena hotel na daraja la Salenda Kumbilamoto, ameuagiza uongozi wa Serena Hotel kupata rangi ya bendere ya Taifa katika vyuma vya barabarani vivyopo karibu na hotel hiyo.
Amesema, kupakwa rangi kwa vyumba hivyo kuta saidia kuwa na mazingira yanayo vitia hasa katika kipindi hiki ambapo Tanzania imekuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa nchi wanachama wa nchi za kusini mwa Africa SADC.
Pamoja na hayo Meya huyo, amewataka wananchi wa Manispaa ya Ilala kuweka mazingira safi na kujitokeza kwa wingi Katika kuwapokea wageni hao na kuchangamkia fursa za biashara.
Post a Comment