Kenya yashinda kura ya Afrika kutafuta kuwa mjumbe asiye wa kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Kenya imeishinda Djibouti na kupata kura ya Umoja wa Afrika ambayo inatarajiwa kuongeza chachu ya kampeni ya nchi hiyo kuwa mjumbe asiye wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Taarifa
iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo imesema, Kenya
imepata kura 37 dhidi ya 13 za Djibouti wakati wa uchaguzi ulioandaliwa
na Kamati ya Kudumu ya Wawakilishi ya Umoja wa Afrika uliofanyika mjini
Addis Ababa, Ethiopia.
Kenya
inatarajiwa kuungana na Niger na Tunisia ambazo zilichaguliwa mwezi
June kuwa wajumbe wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa.
Rais
Uhuru Kenyatta wa Kenya ameupongeza Umoja wa Afrika kwa kuidhinisha nia
ya Kenya ya kuwa na nafasi kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa, na kuzitaka nchi nyingine wanachama wa Umoja huo kuunga mkono
kenya kupata nafasi hiyo.
Post a Comment