WAZIRI MHAGAMA AWAHIMIZA VIJANA KUWA WAZALENDO KWA NCHI YAO.
Mwambawahabari
Na; OWM – KVAU, Kilimanjaro
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama amewahimiza vijana kuwa wazalendo na kuithamini nchi yao.
Akizungumza wakati wa hafla ya
kuwaaga vijana waliopanda Mlima Kilimanjaro jana tarehe 26 Machi, 2019 Mkoani Kilimanjaro ikiwa ni
kuaadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius
Kambarage Nyerere.
Waziri Mhagama alisema kuwa,
Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere alikuwa kiongozi
mzalendo kwa nchi yake na alijali utu na usawa, hivyo ni vyema vijana na vizazi
vijavyo wakarithishwa falsafa za Baba wa Taifa.
“Vijana mna kila sababu kuyaenzi
matendo ya Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere na Mhasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar,
Abeid Amani Karume kwa vitendo kwa kuwa ninyi ndio nguzo ya Taifa na mnaelewa
vema tulipotoka, tulipo na tunapoenda,” alisema Mhagama
Aliongeza kuwa, Viongozi hawa
hawakuwa wabinafsi kwa kujilimbikizia mali na hawakubagua mtu kwa rangi wala
kabila bali walijenga Taifa na kudumisha amani na moja.
Aliendele kwa kuwapongeza
vijana kwa azma yao ya kuenzi historia na mazuri yaliyofanywa na viongozi hao
kwa kupanda mlima Kilimanjaro na kuwatakia baraka waende na kurudi salama.
“Kitendo hiki ni cha kishujaa
na uzalendo wa hali ya juu kwa Taifa ikiwa ishara ya kumuenzi Baba wa Taifa,”
alieleza Mhagama
Aidha Waziri Mhagama alitoa
rai kwa vijana kuwa wazalendo na kuwasihi wafanye kazi kwa bidii ili kujenga Taifa
kupitia uchumi wa viwanda utakao ifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati
ifikapo mwaka 2025.
Alifafanua kuwa uzalendo
lazima ujengwe sambamba na ujenzi wa uchumi wa Taifa, ulinzi na usalama wa Taifa
na utunzaji wa tunu za Taifa.
Pamoja na hayo, aliwapongeza
na kuwashukuru Viongozi wa Mkoa wa Songwe na Lindi pamoja na uongozi wa Hifadhi
ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) kwa ushirikiano mkubwa na Ofisi yake katika kuwashirikisha
vijana kwenye suala hilo.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya
ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba alisema kuwa tukio hili ni muhimu kwa vijana
kutambua historia na mchango wa Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere katika Taifa.
“Tumieni fursa hii kupitia
vitabu mbalimbali vya kihistoria ili mjifunze mipango, mwenendo na malengo ya Baba
wa Taifa itawasaidia na kuwajengea nafasi nzuri ya kujitambua na kuelewa
historia ya Taifa,” alisema Warioba.
Naye Mkurugenzi wa Maendeleo
ya Vijana, Bw. James Kajugusi alieleza kuwa Baba wa Taifa alianza harakati za
kulikomboa Taifa akiwa kijana na aliendelea kufanya hivyo kwa kuwa hamasisha
vijana kujenga Taifa lao baada ya kupata uhuru.
Post a Comment