Rais Magufuli:niligoma Kuongea na Waziri Mwakyembe Baada Ya Taifa Stars Kufungwa Na Lesotho

Rais
Magufuli amefunga hayo wakati akizungumza na wachezaji wa timu ya Taifa
ya Tanzania, Kamati ya Uhamasishaji ya timu ya Taifa pamoja na Bondia
Hassani Mwakinyo ikiwa ni siku moja baada ya timu ya taifa kufuzu
michuano ya Mataifa Afrika.
"Tangu
tulipofungwa na Lesotho na huku Mil. 50 zangu zikiwa zimeliwa iliniuma
kweli kweli, sikuwahi kuongea na Mwakyembe tangu siku ile hadi leo
nilipompigia, aliniandikia meseji kuwa tuwe na Kombe la Magufuli, kama
ilivyo Kagame Cup, sikumjibu.
“Kabla ya mchezo ule nilizungumza naye akiwa Afrika Kusini akaniambia timu iko safi na mchezo huu lazima tushinde na matokeo yake wakafungwa.”
“Nilikuwa nikiangalia ile mechi naona kuna mapungufu, iliniuma kweli, kwa sababu inaniumiza kweli kwa nchi kama Tanzania yenye watu milioni 55 mnakwenda kufungwa na nchi yenye watu milioni 2,” amesema

Mamilioni
ya watanzania jana walikuwa na furaha kufuatia timu ya taifa ya
Tanzania kuichapa Uganda kwa mabao 3 kwa sifuri na kuifanya Tanzania
kuwa miongoni mwa mataifa manne yaliyofuzu fainali za AFCON
zitakazofanyika Juni 2019, nchini Misri.
Post a Comment