DKT. KIKWETE AMEWATAKA WAZAZI KUTOWAFICHA NDANI WATOTO WENYE USONJI.
Mwamawahabari
Na Maria kaira,Mwambawahabari
Rais Mstafu wa awamu ya Nne,Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amewataka wazazi na walezi kutowaficha ndani watoto wenye Usonji kwa kuwa wanauwezo wa kufundishika.
Akizungumza baada ya matembezi hayo Dkt. Kikwete amesema ugonjwa wa usonji umeenea duniani kote kwa wananchi matajiri na masikini, lakini pia unaitaji uvumilivu kwa wazazi na walezi kwa kuwa ugonjwa huo unaitaji uangalizi wa hali ya juu wakati wote.
" Watoto hao wanategemea sana mapenzi ya wazazi na walezi na jamii kwa ujumla, pia wanategemea kulindwa kwasababu wasipolindwa na kuangaliwa wanaweza hata kujiumiza wenyewe"amesema
Aidha ameipongeza Bodi ya shule ya Al Muntazir ambayo imeanzisha shule maalumu ya watoto wenye mahitaji maalumu ikiwemo Usonji ambao wamekuwa wakiwapatia mafunzo mbalimbali ya vitendo pamoja na Elimu.
Dkt. Kikwete ametoa wito kwa wizara husika ikiwemo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto na makundi mbalimbali kwenye jamii kutambua tatizo hilo na kuchukua hatua ya kutoa elimu kwa jamii,katika kuelimisha malenzi kwa watoto hao na nini kifanyike ili kuweza kuwasaidia watoto wenye maradhi ya Usonji.
Aidha amesema jitihada hizo ziongezwe mara dufu kwa kuwekeza elimu kwa jamii ili waweze kutambua ugonjwa wa Usonji,pia ameiomba jamii kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na shule ya Amsen ili mradi huo uweze kufanikiwa.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Shule za Al Muntazir Imtiaz Halji amesema njia bora ya
kuwaonesha watoto wenye mahitaji maalumu ni kuwalinda na kuwapenda na kuacha
tabiya ya kuwatenga ili wasishirikiane na wenzao.
“Wakati sasa
umefika tuunganishe nia zetu kuelekea lengo moja,kufanya kila kitu kilicho
ndani ya uwezo wetu kuunga mkono katika kuelimisha jamii ”amesema
Post a Comment