Tuzo 30 za Tamasha la Filamu la Kimataifa (SZIFF) kutolewa Februari 23 Mlimani City
Hussein
Ndubikile
Mwamba wa
habari
Jumla ya
Tuzo 30 za Filamu zinatarajiwa kutolewa
katika Tamasha la Filamu la Kimataifa la SZIFF litatalofanyika kwenye Ukumbi wa
Mlimani City jijini Dar es Salaam Februari 23 mwaka huu.
Akizungumza
na wanahabari leo jijini humo Mkurugenzi
Uendeshaji vipindi wa Televisheni ya Azam, Yahaya Mohamed amesema kwa takribani
mwezi mmoja na nusu Chaneli ya Sinema Zetu ilionyesha filamu zote zilizopita
duru la kwanza ambapo 237 zilionyeshwa zikijumuishwa filamu ndefu, fupi,
tamthiliya pamoja na makala.
Ameabinisha
kuwa tuzo za SZIFF zimegawanyika katiika makundi mawili zikiwemo za Swahili
Panorama ikijumuisha filamu zote zilizosajiliwa moja kwa moja katika tuzo hizo huku kundi la pili
likijumuisha World Cinema zilizosajiliwa zikitumia lugha ya kigeni zikiwa na tafsiri
ya Kiingereza hususan kwa zile ambazo
hazikuandaliwa kwa lugha hiyo.
“ Tamasha la
SZIFF leo linatangaza filamu zilizopita
katika mchujo wa mwanzo ili kuwania tuzo za sinema zetu kwa mwaka huu,”
amesema Mohamed.
Amesisitiza
kuwa katika kuhakikisha tamasha hilo linakuwa karibu na watazamaji na kupanua
wigo wa ushindani miongoni mwa wasanii na wadau wa sanaa Afrika wameongeza
vipengele viwili vipya kikiwemo kipengele cha Tamthiliya na World Cinema.
Amefafanua
kuwa katika kipengele cha Tamthiliya tuzo zitakazoshindaniwa ni Tuzo ya Tamthiliya
bora, Muongozaji bora, Mwandishi bora, Mhariri bora wa picha jongevu huku za
world cinema zitakuwa ni mtunzi bora wa muziki asili pamoja na mpiga picha
bora, Muigizaji bora wa kike na kiume na filamu bora.
Amesema
washindi watapata zawadi kati ya Sh milioni moja hadi milioni 5 kulingana na
ukubwa wa tuzo pamoja na cheti cha tuzo hizo huku akibainisha upatikanaji wa
washindi wa kila kipengele watakaowania tuzo 30 umegawanyika katika sehemu
mbili wakiwemo washiriki waliochaguliwa na Jopo la Majaji kwa kuzingatia vigezo
na mashati na kwamba sehemu ya pili ni washiriki waliochaguliwa na watazamaji
kupitia tovuti na ujumbe wa meseji.
Kwa upande
wake Mratibu wa tamasha hilo, Sophia Mgaza amesema mwaka huu kumekuwa na
mafanikio makubwa kwani filamu nyingi za mikoani zimeingia duru la pili tofauti
na mwaka jana ambapo zilitoka Dar es Salaam.
Amezitaja
miongoni mwa filamu zilizoingia duru la
pili ni Iyango, Petu na Guru, Siyabonga, Kiumeni, Mama Afrika, Dema,
Safari pamoja na T-Junction.
Nyingine upande wa filamu za vichekesho ni Kazoa ndani ya Imani, Mama Mwali, Mchumia pamoja na Mwali wa Kijiji.
Sophia
amesema filamu zilizoingia duru la pili zitaanza kuonyeshwa leo Saa 10 jioni
katika Chaneli ya Sinema Zetu.
Naye
Mwenyekiti wa Jopo la Majaji, Profesa Martin Mhando amesema upatikanaji wa
washiriki katika kila kipengele umezingatia vigezo vingi na kwamba filamu
zlizoshinda duru la pili ni zile zenye ubora wa hali ya juu.
Pia
ameongeza kuwa mwaka uliopita Rais wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete
alikuwa mgeni wa heshima katika hafla ya tamasha hilo lililovutia wengi
na kwamba kwa mwaka huu mgeni rasmi bado hajawekwa wazi.
Post a Comment