Ads

Naibu Meya Ilala kuzindua semina ya Guru Planet.



Mwambawahabari
Na Heri Shaban
NAIBU MEYA wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto anatarajia kuzindua semina ya Kampuni ya Guru Planet  February 28 katika ukumbi wa NSSF Ilala.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Kampuni ya Guru Planet kwa dhumuni la kuwapa elimu ya usindikaji vyakuka na vipodozi kwa Wajasiriamali wa Wilaya ya Ilala ili waweze kupata masoko.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam Leo Mkurugenzi wa kampuni ya Guru planet Nickson Martin alisema  dhumuni la semina hiyo  ya Wajasiriamali wa Wilaya ya Ilala  imewashirikisha Shirika la Viwango Tanzania (TBS)Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA, ) (SIDO) na  (GS1)kutoa elimu ili iweze kuwatambua watakao kidhi vigezo waweze kupata vibali vya Serikali.

"Semina hii ya February 28 tumezishirikisha  taasisi za Serikali zinazotambua ubora wa bidhaa ili waweze kutoa elimu na kuwatambua rasmi Wajasirimali wa Manispaa ya Ilala "alisema Martini

Martini alisema  katika Wilaya ya Ilala kuna Wajasiriamali wengi wanashindwa kupata masoko makubwa kutokana na wengine bidhaa zao azijatambulika na Serikali hivyo aliwataka Wafanyabiashara wa Wilaya hiyo wale watakao shiriki wajisajili katika ofisi  za kumpuni hiyo .

Martini alisema semina hiyo kwa kila mshiriki kujiunga shilingi 20,000 mshiriki atapewa Cheti na Chakula katika semina hiyo.

Alisema "kauli mbiu kwa Mwaka huu rasimisha bidhaa kwa Ustawi wa Biashara yako jali afya ya watumiaji kwa kuzalisha Bidhaa zilizothibitishwa na mamlaka husika "


No comments