HATUTAMVUMILIA ATAKAYEHUJUMU MKAKATI WA KUFUFUA ZAO LA MICHIKICHI -MAJALIWA
Mwambawahabari
......................................................
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitomvumia mtu yeyote
atakayebainika kuhujumu mkakati wake wa kulifufua zao la michikichi nchini.
Amesema
wanataka kuona wakulima zao hilo wakinufaika kama wengine wa mazao
makuu ya biashara, hivyo haitomfumbia macho mtu atakayezembea.
Aliyasema
hayo jana jioni (Jumapili, Februari 17) mara baada ya kukagua shamba la
michikichi la kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Bulombora.
Alisema
Serikali inataka kuona wakulima wa zao hilo wakinufaika kama ilivyokuwa
kwa wakulima wa korosho, chai, kahawa, pamba na tumbaku.
Alisema
Serikali imeamua kulifufua zao hilo kwa lengo la kumaliza tatizo la
upatikanaji wa mafuta ya kula kwani inatumia fedha nyingi kuagiza nje ya
nchi.
Waziri
Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaagiza viongozi mkoani Kigoma kwamba suala
la kilimo cha michikichi liwe ajenda ya kudumu kwenye vikao vyao.
Kadhalika,
Waziri Mkuu aliiagiza Wizara ya Kilimo ianzishe shamba darasa la zao la
michikichi ili wananchi waweze kujifunza mbinu bora za kulima zao hilo.
Awali,
Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba alisema Serikali imetenga zaidi ya
sh. bilioni 10 kwa ajili ya kuboresha kilimo cha zao la michikicho.
Waziri
huyo alisema kiasi hicho cha fedha kimetengwa katika bajeti ya wizara
hiyo ya mwaka 2019/2020 kwa ajili ya kuboresha kilimo cha michikichi
nchini.
Alisema
iwapo kilimo cha zao hilo kitaboreshwa kitasaidia Serikali kuokoa fedha
nyingi za kigeni zilizokuwa zikitumika kuagiza mafuta kutoka nje ya
nchi.
Pia,
Waziri Mgumba alisema tayari wizara hiyo imeshaongeza watafiti zaidi ya
10 wa zao la michikichi katika kituo cha utafiti wa zao hilo cha
Kihinga.
Waziri
Mgumba alipongeza Jeshi la Magereza na JKT kwa ushirikiano wanaoutoa
kwa wizara katika kipindi hiki cha ufufuaji wa zao la michikichi.
Naye
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi
alimuhakikishia Waziri Mkuu kuwa maelekezo yote aliyoyatoa kuhusu kilimo
cha michikichi watayatekeleza.
Post a Comment