DC ,SARAH MSAFIRI AZINDUA KAMATI YA AMANI KIGAMBONI ,AYATAJA MAJUKUMU YAKE.
Na.John Luhende
Mwamba wa habari
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Sarah Msafiri , ameishukuru kamati ya amani ya
viongozi wa Dini Wilaya ya Kigamboni, kwa kufanya uchaguzi wa viongozi kwa amani na utulivu ,na kusema kuwa kamati
hiyo itasaidia kutatua migogoro inayohusu dini na dini , madhehebu ya dini na migogoro ya kijamii kwa njia ya amani .
DC Msafiri ameyasema hayo
mara baada ya kukamilika kwa tukio la uchaguzi huo, ambao yeye kama
mlezi wa kamati hiyo amesema kamati hiyo
itakuwa kiungo muhimu kati ya serikali
na dini .
“Lengo kubwa la kamati hii ni kuhakikisha tunaimarisha amani ya Wilaya na kuangazia
maeneo yote yenye viashiria vya uvunjifu
wa amani baina ya Madhehebu ama dini na dini, pia inaweza kuishauri serikali
katika mabo mbalimbali , mi niwapongeze kwakumaliza zoezi hili kwa amani bila
mivutano ‘’Alisema
Aidha DC Msafiri amesema hivi karibuni Wilayani humo kumekuwa na migogoro baina ya
dini na Madhehebu ambapo nivigumu kuitatua kisheria ispokuwa kwa mazungumzo ya
ndani kiimani .
“Kuna mambo hayihitaji sheria katika kuya tatua nimambo
ya kiimani zaidi kamati hii itakuwa inasaidia
katika mambo kama hayo”Alisema.
Kwa upande wao viongozi walichaguliwa wametoa ujumbe kwa
jamii na wakisisitiza katika kudumisha
amani na kuvumiliana katika mambo wanayo
hitilafiana Mwenyekiti wakamati hiyo anatoka katika Dini ya Kiislam, Shekhe
Iddi Mtitu ambaye ni shekhe mkuu wa wa Wilaya ya Kigamboni, amesema wanadamu
wote ni watoto wa Mama mmoja wanatakiwa
kuishi kwa maelewano.
“Wanadamu huwa tuna kosea niMwenyezi Mungu pekee asiye
kosea tuna paswa kuvumiliana katika
tofauti zetu kwa yale tunayohitilafiana ili tudumishe amani yetu “Alisema .
Naye katibu wa kamati hiyo ambaye anatoka katika Dini ya
Kikristo Padre Emmanuel Hakiebangimane ,wa parokia ya Mtakatifu Consolata
Kigamboni amewataka wananchi na waumini wa dini zote kuishi kwa umoja
ushirikiano ,upendo na uaminifu.
Post a Comment