CHADEMA WAINGILIA KATI KAULI YA WAZIRI LUGOLA KWA TUNDULISU.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema wamemjibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ambaye jana amemtaka, Tundu Lissu kurejea Tanzania kusaidia upelelezi wa tukio lake la kushambuliwa na risasi.
Lissu
alishambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 nje ya nyumba aliyokuwa akiishi
jijini Dodoma Septemba 7, 2017 na jana Lugola katika mkutano wake na
wanahabari jijini Arusha, alimtaka mbunge huyo wa Singida Mashariki
(Chadema), kurejea nchini kwa kuwa yeye na dereva wake ni mashahidi
muhimu.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mkurugenzi wa
operesheni na mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila amesema chama hicho
kimepokea kwa masikitiko kauli ya Lugola.
Amesema wanaotakiwa kufanya uchunguzi na kutoa majibu ya suala hilo ni Jeshi la Polisi.
Kigaila
amesema kazi ya kukamata, kuchunguza na kufikisha mahakamani ni ya
Serikali na kwamba Lugola alitakiwa kuwaeleza Watanzania nini Serikali
imekifanya kuchunguza tukio hilo.
"Atuambie
(Lugola) anamtaka Lissu arudi kwa document (nyaraka) gani ya kiofisi au
anataka tuanze kufanyia kazi mambo ya mtaani,” amehoji.
Kigaila
amesema kwa mujibu wa maelezo ya Lugola, Serikali haiwezi kuchunguza
tukio ambalo mhusika yupo nje ya nchi, akibainisha kuwa kuna matukio
mengi yamewahi kuchunguzwa wakati wahusika wakiwa hawapo.
"Wakati
Lissu anapigwa risasi hao walinzi wa kampuni binafsi walikuwa wapi?
Lugola awaeleze Watanzania hao anaowaita walinzi binafsi wanaolinda
nyumba hizo walichukua hatua gani? Hao ndio walitakiwa kuwa wa kwanza
kueleza,” amesema.
Post a Comment