Waziri Ummy: ifikapo mwaka 2020 katika wagonjwa 100 wa Kifua Kikuu tutawaibua 70 na kuwapatia matibabu
Hussein
Ndubikile
Mwamba wa
Habari
Serikali
imesema ifikapo mwaka 2020 imejiwekea mikakati kuhakikisha katika kila wagonjwa
100 wa Kifua Kikuu inawaibua wagonjwa 70
na kuwapa matibabu huku ikibainisha takwimu za kiduania mwaka jana zinaonyesha
watu 154,000 kila mwaka huugua ugonjwa huo.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kabla ya Hafla ya kukabidhi Magari 10 na
Pikipiki 35 ambazo zimekabidhiwa kwa Waratibu Halmashauri na Waganga wa Mikoa
kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa Kifua Kifuu na Ukoma.
Amesema kuwa
Tanzania katika mapambano ya ugonjwa imeonyesha nia ya dhati na kwamba mwaka
2020 watahakikisha kati ya wagonjwa 100 wa ugonjwa huo wanafikiwa na kupewa
tiba.
“ Mgonjwa wa
kifua kikuu asipoptaiwa tiba ana uwezo wa kuambukiza watu 20 kila mwaka hadi
tumefanikiwa kupunguza ugonjwa kwa asilimia 44 huku asilimia 56 wako katika
nyumba, vijiji, mtaani na maofisini,” amesema waziri Ummy.
Amebainisha
kuwa kwa asilimia 85 Serikali inatumia vifaa vya sampuli za kutolea majibu ya
ugonjwa huo ndani ya saa mbili na kwamba katika wagonjwa 100, wagonjwa 90 wanatumia dawa.
Amesisitiza
kuwa magari na pikipiki hizo zitacahangia kuongeza nguvu kwa waratibu na
waganga katika mapambano ya ugonjwa huo.
Waziri Ummy
amesema kuna wagonjwa 2000 wa ugonjwa wa ukoma katika halmashauri za Liwale,
Nkasi, Kilombero, Mvomero, Nachingwea, Pangani na Korogwe.
Amewataka
wakuu wa shule za bweni za Serikali na Binafsi kuacha kupokea wanafunzi ambao
hawana fomu za matokeo ya ugonjwa wa kifua kikuu na kuwaagiza waganga wa mikoa
kwenda kufanya ukaguzi wa fomu za wanafunzi.
Ameitaja
miongoni mwa mikoa iliyokabidhiwa magari ni Pwani, Ilala, Songwe, Kilimanjaro,
Tabora na Rukwa.
Halmashauri
zilizokabidhiwa pikipiki ni Ngara, Urambo, Nzega, Ujiji, Mbulu, Hanang, Msalala,
Kilolo, Amana, Mbagala, Mburahati, Tanga, Muheza, Kilombero na Gairo
Kwa upande
wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Ujerumani-Tanzani linalojishughulisha
na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu na Ukoma (GLRA), Burchard Rwamtoga
amesema asasi hiyo ilianza kazi ya
kusaidia wagonjwa huo na ukoma mwaka 1959 na kupata usajili mwaka 1977.
Amesema
asasi hiyo hushirikiana kwa miaka mitano mitano na serikali na kwamba
makubaliano ya sasa ni kuanzia mwaka 2015 hadi 2020.
Burchard
amebainisha katika kipindi cha miaka 21
wamesaidia Mpango wa Kudhibiti
Kifua Kikuu na Ukoma magri 270 kwa waratibu wa mikoa na pikpiki 675 kwa
waratibu wa mikoa.
Pia amesema
mwaka 2018 GLRA limesaidia kununua magari 9 aina ya Toyota Landcruiser Hard
Top, gari moja Suzuki Jimny na Pikpiki 35 aina ya Honda XL 125.
Ametaja
gharama za magari 9 ni Sh 661,370,760 bila uhuru huku Suzuki Jimny ni Sh
30,485,000/- bila ushuru huku akibainisha Pikipiki 35 zimegharimu Sh
221,047,016 (bila ushuru).
Katika hatua
nyingine amesema magari 10 yaliyokabidhiwa yote yamekatiwa bima kubwa kwa
kipindi cha mwaka mmoja.



Post a Comment