Ads

TAMASHA SAUTI ZA BUSARA KUKUZA UTAMADUNI WA KIAFRIKA.

Balozi wa Norway nchini Tanzania, Bi. Elisabeth Jacobsen akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu tamasha la busara linalotarajia kufanyika Zanzibar. 
Mkurugenzi wa Tamasha la Busara, Yusuf Mahmoud akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuelezea jinsi walivyoweza kujipanga kuwapa burudani kwa washiriki wa tamasha hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Tamasha la Busara Bi. Julia Bishop (wa tatu toka kulia) akizungumzia jinsi ambavyo Tamasha hilo limekuwa msaada mkubwa katika kutangaza utamaduni wa mwafrika. Wengine ni Mkurugenzi wa Tamasha la Busara, Yusuf Mahmoud (kwanza kushoto), Balozi wa Norway nchini Tanzania, Bi. Elisabeth Jacobsen na Meneja wa Tamasha la Busara Journey Ramadhani.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Tamasha la sauti za busara linalotarajiwa kufanyika Zanzibar February I7 hadi I0 mwaka huu linatarajiwa kuwa na msaada mkubwa katika kukuza utamaduni wa kiafrika kwenda mataifa mbalimbali duniania 

Tamasha hilo la  16 la sauti za busara litawakutanisha  wasanii kutoka maeneo mbalimbali kupitia orodha ya wasanii ambao watanogesha watazamaji wa aina mbalimbali ya muziki .

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Yusuf Mahmoud, amesema kuwa tamasha la sauti za busara litasaidia kupanua wigo wa kutangaza utamadunia wa kiafrika katika maeneo mbalimbali duniani.

Amesema kuwa ni vizuri wadau mbalimbali wakajitokeza kushiriki katika tamasha hilo kutokana na wasanii waliochaguliwa kushiriki ni wabunifu katika tasnia ya Sanaa.

“Tunawakawakaribisha wapenzi wa muziki kutoka maeneo yote  ya dunia,wakijumuika pamoja kusherehekea upekee wa sauti kutoka nchi ya Algeria hadi Zimbabwe  kutoka cape Town hadi Casablanca ” amesema  Mahmoud.

Mahmoud ameeleza kuwa lengo la  tamasha hilo ni kuwatangaza wasanii wachanga na wale wanaochipukia kutoka Afrika mashariki. 

Hata hivyo amewataka wadau mbalimbali washiriki katika tamasha hilo, huku akiwataja baadhi ya bendi ambazo Itashiriki ikiwemo bendi kama  wamwiduka kutoka Mbeya  na Skide kijana anayefanya muziki wa aina ya singeli ambao asili yake halisi ni Tanzania na kwa sasa unakaribia kuuteka ulimwengu.

 Amesema luwa lengo la kuwepo tamasha la sauti za busara si tu kwa ajili ya kuburudisha watu bali pia kueleimisha jamii na kuangaza maovu yanayoletwa na rushwa likiwa kama tatizo linaloendelea kuwanyima vijana haki zao za kimsingi na hasa wanamuziki wa kike. 

Hata hivyo  Meneja Journey Ramadhan, amesema kuwa tamasha la sauti za busara litaendelea kufanya vizuri katika  linatangaza Tanzania na Zanzibar na ulimwengu kote kupitia sanaa ya muziki.

Ramadhan ameeleza kuwa tamasha hilo linawavuta karibu waandaji wa matamasha wa kimataifa kwa kuwapa  fursa ya wanamuziki wa KIAFRIKA  kuwasilisha kazi zao.

Amsema kuwa orodha ya mwaka huu kuna wasanii kama Fid Q, Damian Soul, Mkubwa na Wanawe Crew, Stone Town rockerz, Tausi Women’s Taarab, Rajab Suleiman, Kithara, Afrigo band, Jackie Akello na Eli Maliki (Uganda) Fadhilee Itulya na pamoja na Shamsi Music kutoka Kenya.

Tamasha la sauti za busara linadhaminiwa na ubalozi wa Norway, Ubalozi wa Uswis nchini Tanzania na Zambia, Umoja wa Ulaya, Africalia, Ubalozi wa Ujerumani  na Shirika la Ethiopia pamoja na Zanzibar Media Corporation ili kuhakikisha sanaa inapiga hatua.

Washiriki wa tamasha la sauti za busara wanaweza kununua teketi kupitia mtandao wa  www.busaramusic.org

No comments