TAMADUNI ZENYE MADHARA ZALETA ATHARI KWA WANAWAKE MKOANI MARA
Na Anthony Ishengoma-Mara.
Jamii mkoani Mara bado
inaendeleza mila potofu ya kuamini kuwa mwanamke asiyekeketwa ni mkosi kwa
familia jambo ambalo linaendeleza vitendo vya kwa ukatili wa hali ya juu dhidi
ya wanawake Mkoani humo.
Akiongea wakati wa ufanguzi wa
Kikao kazi cha uzinduzi wa Kampeini ya kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na
Watoto leo Mkoani Mara Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara
Bi. Karolina Mtaphula amesema inapotokea binti anayekeketwa akapoteza maisha
kutokana na ukeketaji binti huyo amekuwa akitupwa polini bila kuzikwa kwa
taratibu za kawaida kwasababu jamii pia inaamini ni mkosi kwa jamii na kwa
familia yake.
Aidha Bi. Mtapula aliongeza kuwa
Jamii ya Mkoa wa Mara inatakiwa ijilinganishe na mikoa mingine ambayo haina
mila ya ukeketaji ili kujenga ufahamu kuwa wanawake kutoka jamii hizo kama
wamekuwa wakileta mikosi katika familia zao kama amabavyo mila zao inawafanya
waamini.
‘’Wanawake katika Mikoa ambayo
haina ukeketaji wanazidi kupiga hatua za kimaendeleo na kufaidika kielimu
lakini katika Mkoa wa Mara mila potofu imeendelea kurudisha nyuma maendeleo ya
wanawake hivyo nawaomba mlinganishe na jamii hizi kuona kama kweli wanawake wasipokeketwa
wanaleta mikosi’’. Alendelea kusema Bi. Mtapula.
Aidha Bi. Mtapula alisema pamoja
na kuwepo kwa vitendo vaya ukatili amesema vitendo hivyo katika Mkoa wa Mara
takwimu zilizopo zinaonesha vitendo vya mkoani humo vimeanza kupungua kwani kwa
takwimu za mwaka 2010 mkoa huo uliongoza kitaifa kwa kuwa na sailimia 72 lakini
kwa takwimu za mwaka 2015-216 takwimu zinaonesha mkoa umeshuka hadi kufikia
asilimia 55.
Wakati huo huo Mkurugenzi
anayeshugulikia masuala ya watoto Bw. Sebastian Kitiku amewaambia wajumbe wa
kikao kazi hicho kuwa wizara iko mkoani humo kukutana na kujadiliana na
viongozi wa Mkoa na Halmashauri pamoja na viongozi wadini kwa ajili kutengeneza
ujumbe utakaotumika katika kampeini ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.
Amewataka wajumbe hao kutengeneza
ujumbea amabao kimsingi utaendana na mazingira ya Mkoa ikiwemo mila nzuri
zilizopo kwakuwa ujumbe unatumika Mazingira ya Mara unaweza usitumike katika
mikoa mingine kutokana na tofauti za kimazingira.
Kazi ya kutengeneza ujumbe kwa
ajili ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni inaendelea itaendelea katika mikoa
yenye takwimu za juu katika ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambayo ni mikoa
ya Shinyanga, Tabora, Singida na Rukwa.
Post a Comment